Baadhi
ya matukio katika igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs.
Lucy goes to Africa) likiwa limeigizwa na Msanii kutoka Marekani
Bi Toussaint Duchess lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
Agosti 15 . Picha na Raymond Mushumbusi
Mkurugenzi wa Idara ya habari (MAELEZO) Hassan Abbas amesema kuwa ujio wa msanii wa maigizo
kutoka nchini Marekani Toussaint Duchess maarufu kama ‘Mrs. Lucy’ ulete
chachu katika amendeleo ya sanaa kwa
wadau wake hapa nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Nape Nnauye aliyekuwa mgeni
rasmi kwenye uzinduzi wa igizo la Mrs. Lucy linaloitwa ‘Mrs. Lucy Goest to
Africa’ Abbas alisema kuwa ni vyema wadau wa sanaa wakatumia ujio huo kama
changamoto itakayowasaidia kujifunza na kuwa
wabunifu zaidi katika kazi zao za sanaa.
“Ujio wa muigizaji Mrs. Lucy ni changamoto kwa wadau wa
sanaa nchini, ni fursa ya kujifunza kwa wasanii hususani katika eneo la sanaa
za jukwaani, vile vile ni fursa kwa vijana wa kitanzania ambao wanatarajia
kufanya kazi za sanaa” Abbas.
Bongoweekend ambayo ilikuwepo
kwenye onyesho hilo lililofanyika
kwenye ukumbi hapo iliweza kushuhudia
wadau mbalimbali wakifurahia
kutokana na wasanii wa hapa nyumbani kuweza kumudu vyema katika uchezaji wa maigizo kana kwamba walikuwa
wakicheza mtu wa kawaida na siyo yule
msanii nyota Mrs. Lucy kutoka nchini Marekani.
Wasanii ambao wa nyumbani waliong’ara ni pamoja na mama na mwana
waliojikita muda mrefu kwenye
tasnia ya filamu na maigio ambao ni Suzan Lewis (Natasha) na binti yake
Yvone Cherry (Monalisa)ambao
wameshiriki na kuonesha ubunifu na
umahiri wa hali ya juu ikiwa ni pamoja
nha kumleta nchini msanii huyo.
Aidha Abbas ametoa
pongezi kwa kituo cha televisheni cha Azam na wasanii Natasha na Monalisa ambao wameshiriki kwa ubunifu wa kumleta msanii huyo nchini
pamoja na maboresho mengine yaliyoofanywa na Azam.
Azam TV wanatarajia kuonyesha
igizo hilo la msanii huyo kutoka nchini pamoja na filamu mbalimbali zitakazofanywa na
msanii huyo.
0 Comments