DC KISARAWE PETRO MAGOTI ATOA WITO KWA JESHI LA AKIBA KUTO RUBUNIWA NA WANASIASA


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba ambayo yamefanyika leo tarehe 1,Novemba ,2024 Kata ya Manerumango Mkoani Pwani.

Manerumango, Kisarawe 

Mkuu wa Wilaya  ya Kisarawe Petro Magoti amewaasa wahitimu wa mafunzo wa  Jeshi  la akiba kutorubuniwa na wanasiasa mara baada ya kupata mafunzo hayo.

"Msijingize kwenye makundi ya wanasiasa ambao hutumia mbinu za kuwarubuni kwa sababu wanafahamu mmepewa mafunzo ya ulinzi na usalama wa raia nawasisitiza nendeni mkawe  makini na kuzingatia kiapo chenu" amesema DC Magoti.

Nawaahidi kuwa nitawapa kazi hivyo hamtokuwa mkizagaa mitaani Kisarawe  ina kazi nyingi za kufanya hivyo nanyi mnapaswa mkawe wazalendo.

DC  Magoti amesema hayo leo Novemba  Mosi alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kufunga  mafunzo hayo ya jeshi la akiba yamefanyika kwa muda wa  wiki 16 ya kundi la 23  mwaka 2024 ambayo yamehusisha vijana 119.

Akisoma risala   kwa niaba ya wenzake mhitimu  wamafunzo hayo Nasma Hamisi Chingwile amesema kuwa  wanaomba  ziwekwe sheria kali  kwa taasisi mbalimbali ambazo hutoa ajira za ulinzi kwa watu ambao hawajapitia mafunzo na mbinu walizopewa wao.
"Tunaomba serikali  itupe kipaumbele pindi ajira zinapotokea kwenye Majeshi yetu ikiwa pamoja  na Jeshi la Polisi Idara ya Uhamiaji  na JKT "amesema Chingwile.

Wakati huohuo ameongeza kwa kusema kuwa  wakufunzi wao  wawezeshwe  kwa kuboreshewa maslahi mazuri ili waweze kuwafundisha kwa ari zaidi vijana hao wa jeshi la akiba.

Awali akizungumza  kuhusu changamoto  wanaozipitia  kwenye mchakato wa mafunzo Mshauri  wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Kisarawe Meja Silvery Mabubu amemweleza DC Magoti  kuwa wanakabiliwa na ukata wa  fedha za kujikimu kwa vijana wawapo mafunzoni hali ambayo husababisha wakatishe mafunzo na kwenda kufanya vibarua  ili wapate fedha za kununua sare zao.

"Mheshimiwa vijana wetu wanakumbana na changamoto  ya mavazi  jambo linalopelekea baadhi yao kukatisha mafunzo na kwenda kufanya vibarua ili waweze kupata fedha za kujikimu  kwa manunuzi ya sare zao hivyo tunaiomba Halmashauri  ya Kisarawe ilibebe hili jambo hili  ambalo la  muhimu na  lizalendo " amesema Meja Mabubu.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba ambayo yamefanyika leo terehe 1,Novemba ,2024 Kata ya Manerumango Mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Petro Magoti  ambaye alikua  mgeni rasmi kwenye mahafali ya wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba yaliyofanyika leo tarehe 1,Novemba 2024 Manerumango Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.
Baadhi  ya wahitimu wakipita mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro 

Post a Comment

0 Comments