Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo akizungumza kwenye Kisarawe Afya Gala ambayo ni harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi wa jengo jipya la VIP kwenye Hospitali ya Kisarawe, Mkoani Pwani imefanyika tarehe 2 ,Novemba, 2024 kwenye Ukumbi wa Sekondari ya Minaki .
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ambaye piani Mbunge wa Jimbo la Kisarawe akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti mchango wake kiasi cha Mil.6 ikiwa ni katika hatua za awali kuchangia ujenzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti jana Novemba 2 ametembeza bakuli meza baada ya meza kwa wadau mbalimbali ikiwa ni katika kuchangia ujenzi wa jengo maalumu la wagonjwa Hospitali ya Kisarawe Mkoani Pwani.
DC Magoti ameendesha harambee hiyo ambapo ametangaza kukusanya fedha taslimu kiasi cha Ml.100 jambo ambalo linaonesha taswira nzuri katika kufikia lengo la ujenzi jengo jipya na la kisasa linalokadiriwa kugharimu kiasi cha Mil.250 hadi kukamilika.
Aidha mgeni rasmi kwenye hafla hiyo alikiwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo.
Baadhi ya wadau na wakazi wa Kisarawe wakiwa kwenye haflahiyo.Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani kushoto anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wadau mbalimbali wa Kisarawe.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akizungumza kuhusu tathmini ya hafla hiyo amesema kuwa wamepata kiasi cha Mil.100 ambazo wataanza ujenzi wa jengo hilo mara moja.
"Tulikuwa tunahitaji kiasi cha Mi.200 lakini tumepata Mil.100 si haba hivyo tutaanza ujenzi na pindi zitakapoisha tutaitisha harambee ingine ya kuchangia umaliziaji wa jengo hilo" amesema DC Magoti.
Wakati huohuo amesema kuwa wanapokea misaada ya vifaa vya ujenzi ikiwa ni pamoja na mabati,saruji,kokoto michaga na vifaa vyote vinavyohitajika kwenye ujenzi.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Waziri Jafo amesema kuwa anaishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na waratibu wengine kwa kuratibu tukio hilo muhimu pia amefurahi kuona Waalimu wa ngazi za chini kwa namna walivyojitokeza kwa wingi huku akisisitiza kuwa kuna mambo mbalibali ambayo yanahitaji nguvu ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuchangishana katika ujenzi wa nyumba za waalimu huku akisema kuwa milango iko wazi kwa kila mdau kwa sababu lengo ni kuijenga Kisarawe.
0 Comments