NA FRANK MVUNGI -MAELEZO
Taasisi
ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) yabaini kuwepo kwa sukari iliyofichwa
tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda
cha Sukari Kilombero.
Kwa
mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU Valentine Mlolowa Taasisi hiyo imeanza
uchunguzi dhidi ya swala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Taarifa
hiyo imefafanua kuwa mnamo tarehe 05 Mei, 2016 timu ya uchunguzi ilitembelea
maghala yaliyopo Tabata Jijini Dar es salaam na kubaini uwepo wa sukari hiyo.
TAKUKURU tayari imetembelea Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia
ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni
miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na anayetuhumiwa
kuficha bidhaa hiyo. Ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha
uchunguzi uliofanywa na Taasisi hiyo ulibaini
kuwepo kwa njama za dhati za kutouza sukari iliyokutwa katika maghala hayo kulikofanywa
na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hiyo hapakuwa
na dalili za upakiaji wa sukari hiyo ili
iweze kusambazwa.
Taarifa
hiyo imeendelea kufafanua kuwa katika eneo la Kitumbini kumekuwa na wananchi wengi wanaohitaji bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.
Katika
uchunguzi wake TAKUKURU pia imebaini
kuwepo kwa mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa
kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa
hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa
kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko.
Kuficha
bidhaa ni kosa la uhujumu uchumi na ni
kinyume na Aya ya 3 Jedwali la kwanza Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya
200 [Chapisho la Mwaka 2002]. Serikali haitavumilia hujuma za namna hii na itachukua
hatua kali dhidi ya mfanyabiashara yeyote ataekwenda kinyume na sheria hii.
TAKUKURU imetoa wito kwa wafanyabiashara wote wa
sukari kuacha vitendo vya kuficha sukari na vyombo vya uchunguzi vinafuatilia
kote nchini na yeyote atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na mkondo
wa Sheria.
0 Comments