HAFLA YA KUFUNGA KAMBI YA MOYO TAASISI YA JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAFANA


 Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akizungumza na madaktari wa wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar na nchini Uingereza waliokuwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifanya matibabu ya moyo, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Taasisi yake ndio kiungo cha kuunanisha taasisi zilizoshiriki kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

PICHA  ZOTE NA  AVILA KAKINGO .
Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala akizungumza hatika hafla ya kufunga kambi ya madakitari wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar waliokuwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuwaaga madaktari wa nchi hizo.
 Picha ya pamoja ya madaktari bingwa wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti za nchi tatu.


NA  MWANDISHI WETU ,DAR ES SALAAM
 
MADAKTARI wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamefunga kambi ya Madaktari wa tiba ya Moyo wa kutoka Saudi Arabia, Uingereza na Qutar na baaadhi ya madaktari wenye utaalam wa tiba ya matatizo ya moyo hapa nchini.
 
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi  ya Dhi  Nureyn  Islamic  Foundation Said Abri iliyokuwa kiungo  cha kuunganisha  nguvu  baina ya  Taasisi zilizoshiriki  katika kuokoa  maisha ya watoto  waliokuwa wanasumbuliwa na maradhi ya moyo.
 
  Abri akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo  kutoka nchi za Saudi Arabia, Uingereza na Qutar Jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa kambi hiyo imejumuisha pamoja Taasisi nne kutoka nchi tatu tofauti.

Abri alisema Taasisi zilizoshiriki kambi ya Moyo Muhimbili ni Muntada Aid ya Uingereza, Timu ya Madaktari kutoka Saudi Arabia, Taasisi ya Araf kutoka Qutar na taasisi ya Dhi Nureyn ya Iringa  hapa nchini na Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Alsema kuwa kambi  hii ya sasa imefanikiwa kuwatibu watoto wenye matatizo ya moyo 66 ambao walikuwa wamepangwa kusafirishwa  nje ya nchi kwa ajili ya matibabu sasa wametibiwa hapa nchini na kuokoa mabilioni ya fedha za serikali.
 
Kwa upande wake Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo amewashukuru madaktari kutoka taasasisi hizo kwa kuja hapa nchini na kuokoa watoto wenye matatizo ya moyo 200 ambao tayariwametibiwa hapahapa nchini.

Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala akizungumza hatika hafla ya kufunga kambi ya madakitari wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar waliokuwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuwaaga madaktari wa nchi hizo.
 Katibu mkuu na mkurugenzi wa Muntada Aid, Sheikh Khalid Sukeir akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo jijini Dar es Salaam leo.
 Kiongozi wa Madaktari, Jamil Al Ataa akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo jijini Dar es Salaam leo.
 Mwakilishi wa Balozi wa Qatar, Wajih Al Uteibly akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akimkabidhi zawadi ya ngao   Kiongozi wa Madaktari, Jamil Al Ataa wakati wa hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi akikabidhiwa zawadi katika  hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri.

Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala akikabidhiwa zawadi wakati wa hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri.


 
 

Post a Comment

0 Comments