SHEIKH PONDA AMPONDA SHEIKH WA MKOA WA DAR ES SALAAM KWA KUMSINGIZIA SHEIKH FARID

Katibu wa Taasisi za Juiya za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda alipozungumza na waandishi wa habari Jijiji Dar es Salaam leo asubuhi nje ya Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Jijini Dar es Salaam.

Sheikh Ponda amekanusha vikali taarifa zilizotolewa  jana  na Sheikh MKuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa kua wamepokea barua kutoka kwa Kiongozi wa Uamsho Ameir Farid kwamva anaunga mkono kurudiwa uchaguzi wa Zanzibar siyo kweli.

"Kwa niaba ya Sheikha Farid nakanusha taarifa hizo kuwa siyo za kweli , sisi tuliposikia tulifanya uchunguzi wetu kwa kina na kugundua kwamba Sheikh Farid hakuandika barua yeyote na wala hajamtuma mtu  hii ni kutokana  na kua mfungwa yeyote hawezi kufanya jambo bila mkuu wa magereza kujua kadhalika tumeongea na wakili wake na yeye amekanusha taarifa hizo zilizotolewa kuwa hasina ukweli wowote na mteja wake hajawasiliana  ama kutoa  taarifa zozote zile" alisema Ponda.

 Jana Sheikh Mussa aliwaanbia waandiahi wa habari kwamba  Sheikh Farid ambaye yuko gerezani ameandika barua ya kuunga mkono kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.

1. Uchaguzi Wa tarehe 25.10.2015 kwa pande zote za muungano uliosimamiwa na NEC na ZEC ulikuwa halali na mchakato wake kama zilivyo ripotiwa na  waangalizi kwa ujumla ulikwenda vizuri sana.

2. Rais  Wa muungano wabunge na madiwani wamepatikana kwa uchaguzi huo. Sehemu ya Zanzibar  Wabunge  wa   Bunge la Jamuhuri ya Muungano  wa Tanzania wamepatikana kwa uchaguzi uliosimamiwa na ZEC na matokeo yake tunayahesjimu.

 Hatahivyo kwa sababu ambazo hazina msingi wowote mwenyekiti Wa ZEC walifuta uchaguzi wote wa kuwapata viongozi wa  Zanzibar. Hatua ile haikuwa halali kwa kwa sababu mbili Kuu:-
A. Tume baada ya kutoa matokeo haina mamlaka kisheria kufuta matojeo.

B. Uamuzi wa kufuta matokeo hata kama tume  ingekuwa na mamlaka maamuzi yale hayakuwa ya tume bali ni maamuzi ya mtu mmoja.

Kwa sababu hizo uchaguzi wa Zanzibar na matokeo yake bado ni halali na kurudia uchaguzi ni kosa na ni kupanda mbegu mpya ya chuki miongoni mwa wananchi.

Hata hivyo tunaunga mkono hatua za mwanzo zilizochukuliwa kunusuru hali ya kisiasa Zanzibar kwa kufanya mazungumzo baina ya vyama hasimu vya CUF na CCM.

Pia tunaunga mkono ahadi ya Rais  Dk.  John Magufuli kushughulikia mzozo huu aliyoitoa bungeni kuwa atashirikiana na maalim seif, na Dk. Shin kupata suluhu.

Mpaka sasa watanzania hatujaambiwa kwa taarifa ya pamoja kutoka ccm na CUF mazungumzo waliyofanya yameishia wapi yapi wamekubaliana na yapi hawajakubaliana na nini hatima ya mazungumzo yao.

Pia rais hajatupa taarifa amefikia wapi katika ahadi yake ya kushirikiana na Maalim Seif na  Shein kuumaliza mzozo huu.

Tunapinga vikali uamuzi  wa ZEC kutangaza tarehe ya kurudia uchaguzi kabla ya kupatikana kwa  ufumbuzi wa mambo ya msingi na ya kisheria kupatikana.

Hali hiyo inaweza kuleta fujo hasama na kuharibu utangamano uliopatikana kwa kipindi cha miaka ya karibuni znz.

HIVYO TUNASHAURI YAFUATAYO:

1.Rais atimize ahadi yakw aliyoitoa  bungeni  na kwa vitendo  na kuhakikisha anamaliza mzozo huu na anaupatia ufumbuzi bila kuitumbukiza Zanzibar   kwenye dhiki  na uhasama ulio pelea.

2. Kwa kuwa usalama ni suala la Muungano  na majeshi  yaliyoko Zanzibar yako  pale  kwa matakwa na amri ya rais hivyo asochua hatua   ya kuumaliza mzozo huu kwa njia ya kuafaka  matatizo yatakayotokea hayoweza kukwepa lawama na kuwajibika.

3. Vyama vya siasa,msajili wa  vyama hivyo   na wananchi wote wakemee  na Chama Cha Mapinduzi  (CCM) wafute kauli zake zilizotolewa na baadhi ya wanachama wake  ikiwemo bunge la katiba kuwa  CCM haitaitoa serilali ya Zanzibar kupitia sanduku
la kura . Kauli hii inaweza kuwa ndiyo msingi wa  msingi wa kufuta uchaguzi wa Zanzibar.

MWISHO KWA NIABA YA SHEIJH FARID TUNAKANUSHA NADAI KUWS SHEIKH ANESHAURI JUTUDIWS UCHAGUZI. NADAI GAYO HAYANA MSINGI KWA MUJIBU WA MAELEZO ALIYOTUPA. GAJAWAHI KUMTUMA MTU YEYORE ATOE TAARIFA HIYO

Post a Comment

0 Comments