Dokta Manyaunyau katika pozi .
Na Mwandishi wetu , Dar es Salaam
Mdau wa masuala ya
mbalimbali ya burudani ,muziki , filamu na sanaa mbalimbali nchini ambaye pia ni mganga wa tiba za asilia Jongo Selemani almaarufu kwa jina la ‘Dk
Manyaunyau amejitokeza hadharani
kujisafisha juu ya kuchafuliwa jina lake kuwa kafungwa jela.
Akizungumza na Bongoweekend maeneo ya Mlimani City , jijini Dar es
Salaam hivi karibuni alisema kwamba kutumika vibaya kwa
jina lake kumemleta usumbufu mkubwa ikiwa ni pamoja na kukimbiwa na
wateja wake wapya na wa zamani
wakimhofia kwamba yeye ni tapeli jambo ambalo
halina ukweli wowote.
“Mimi niko uraiani na sina tuhuma zozote ilitokea tu mtu
akawa anafanya shughuli zake akatumia jina langu kwa makosa mimi jina hili
nimelisajili na ninalilipia kodi hivyo inauma sana kuona mtu mwingine
analitumia kwa maslahi yake binafsi sasa ona ameniletea matatizo makubwa nimekimbiwa na wateja wangu ” alisema Mnayaunyau.
“Awali nilipuuzia na kuona kwa sababu wale watu ambao
walikuwa washitakiwa katika kesi iliyokua ikiunguruma katika mahakama ya Ilala , alikana kuwa yeye hakujipa jina hilo la 'Manyaunyau' bali alipewa na wateja wake aliokuwa akiwatibu.Lakini kusema kweli hivi sasa kashfa hiyo inanigharimu sana”
alisema Manyaunyau huku akionesha sura yenye huzuni kwa mwandishi.
Aliongeza kwa kusema kuwa anawasihi wateja pamoja na mashabiki wake kuwa yeye bado yupo katika ofisi zake zilizopo Tabata Mawenzi na anaye mhitaji anaweza kumfuata na atapata
huduma kama kawaida.Manyaunyau amekuwa mdau mkubwa wa sanaa kutokana na kutoa
ufadhili na kuwasaidia wasanii wengi katika nyanja mbalimbali kwa lengo la
kuinua sanaa nchini.
0 Comments