BONDIA VICENT MBILINYI HAPANIA KUMCHAKAZA DEO NJIKU DESEMBA 25 MOROGORO



Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimnowa bondia Vicent Mbilinyi wakati wa maandalizi yake ya mwisho kucheza na Deo Njiku Desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Vicent Mbilinyi akielekezwa jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi yake ya mwisho kwa ajili ya kupambana na Deo Njiku desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea na mazoezi yake ya mwisho kwa ajili ya mpambano wake wa Desemba 25

kwa ajili ya kupambana na Deo Njiku mpambano utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro

mpambano uho wa raundi sita umekuwa na kivutio kikubwa
Mvuto wa pambano hilo unatokana na ukweli kuwa, linakutanisha mabondia wa vizazi tofauti, Mbilinyi akiwa ni bondia wa kizazi cha sasa, wakati Njiku akiwa mmoja wa mabondia wakongwe.
 uku Mbilinyi akiwa chipkizi  ambapo alisema maandalizi yake ni ya hali ya juu, nia ikiwa ni kuhitimisha utawala wa mabondia wakongwe.
"Niko kwenye mazoezi makali, chini ya kocha wangu Rajabu Mhamila 'Super D'. Nia ni kushinda pambano hilo na kuimalisha rekodi yangu ya mapambano niliyoshinda.
"Lakini pia, nataka kuhakikisha namchapa Njiku, ili sio tu kujenga heshima yangu, bali pia kumaliza utawala wa mabondia wakonge nchini. Hii itaongeza molari miongoni mwa mabondia vijana nchini," anasisitiza Mbilinyi


ambaye anatokea katika kambi ya Super D Boxing Promotion inayozalisha na kukuza vipaji vya vijana mbalimbali nchini na kuviendeleza katika mchezo wa masumbwi
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Post a Comment

0 Comments