KAMATI TAIFA STARS YATAMBULISHWA RASMI


Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa Stars iliyoteuliwa hivi karibuni na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bwana Farough Baghozah leo hii amekutana na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kuitambulisha rasmi kamati hiyo.


Katika kamati hiyo ya Taifa ya Stars wapo Michael Wambura – Makamu Mwenyekiti, Bi Teddy Mapunda – Katibu, Wakili Imani Madega – Mweka Hazina, na wajumbe wengine ni Juma Pinto, Isaac Chanji, Salum Abdalla na Moses Katabaro.

Pia Mwenyekiti amechukua fursa hiyo kutangaza kamati ndogondogo na wajumbe wake kama ifuatavyo:

 1. Maandalizi ya timu, zikiwemo huduma kwa timu ya Taifa stars

 Mwenyekiti – Imani Madega

 Wajumbe – Msafiri Mgoyi,Teddy Mapunda.

2. Uhamasishaji wa mchezo (Michezo ijayo) na Masoko

 Mwenyekiti – Juma Pinto

 Wajumbe – Baraka Kizuguto, Mlamu Ng’ambi, Charles Hamka, Hashim  Lundenga, Maulid Kitenge, Shaffih Dauda, Salehe Ally, Peter Simon,  Edo Kumwembe na Mahmoud Zubeiry.

 3. Kamati ya Fedha

Mwenyekiti – Farough Baghozah

Wajumbe – Teddy Mapunda, Michael Wambura, Imani Madega,   Juma Pinto,  Isaac Chanji, Moses Katabaro na Edgar Masoud.

4. Mikakati ya ushindi – itakuwa na kamati ndogondogo na zitakuwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti Farough Baghozah, Teddy Mapunda, Mohamed Nassoro, Philemon Ntahilaja, Isaac Kasanga, Cresencius Magori.

Pia kamati imetangaza kauli mbiu ya ushindi inayosema “NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU” itakayoanza kutumika kuanzia leo hii.  Pia Kamati imemteua Bi Teddy Mapunda kuwa msemaji mkuu wa kamati hiyo.

Timu inatarajia kuweka kambi Nje ya Nchi kwa takribani siku 12 ili kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria Novemba 14 Dar es salaam, na Novemba 17 nchini Algeria.

Aidha Mwenyekiti alitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania wote warudishe imani kwa timu yao, wajitokeze kwa wingi kwenye mechi ijayo tarehe 14 November dhidi ya Algeria hapa nyumbani.  Pia akatoa wito kwa Watanzania Wote kuchangia timu kwa hali na mali (Madawa, Maji, vifaa vya michezo na kadhalika)…aliongeza ‘Mwenyekiti wa Kamati Bwana Farough Baghouzah.


Post a Comment

0 Comments