MWANAMUZIKI
nyota wa kike anayetamba na kibao kinacho lalama kuhusu mapenzi, ‘Posa ya
Bolingo’ Alicious Theluji pichani juu, anatarajiwa kupamba onyesho la ‘Usiku wa Masauti’
litakalofanyika jijini Dar es Salaam ,
Aprili 18 mwaka huu.
Alicious
mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC), aliyezaliwa Jimbo la Kivu, alihamia na familia yake nchini Kenya wakati akiwa na miaka minne na kwa sasa
yuko nchini Sweden
kimasomo.
Mbali
na Posa ya Bolingo, nyimbo nyingine za Alicious ni ‘Niko Poa’, ‘Mpita
Njia’ aliomshirikisha Juliana Kanyamozi
wa Uganda ,
ambazo ameziimba kwa Kiswahili.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam mwanamuziki wa kujitegemea ‘Solo
Artist’ Christian Bella ‘Kijana wa Masauti’ alisema taratibu za kumleta msanii
huyo zimekamilika, kinachosubiriwa ni muda tu ufike, ambako viingilio na ukumbi
vitatangazwa.
Alisema
Alicious ataingia nchini wiki moja kabla na watafanya naye mazoezi ya pamoja
ili siku ya Usiku wa Masauti, mashabiki wapate burudani ya hali yajuu.
Bella,
alisema Alicious amefurahi kualikwa kuja kunogesha usiku huo, ambako pia
ataimba ‘live’ kwenye onyesho hilo
ambalo Bella amepanga kuzindua rasmi video ya wimbo wake wa ‘Nashindwa’
aliourekodi nchini Afrika Kusini.
Bella,
alisema ana imani kubwa video hiyo ya ‘Nashindwa’ italeta mapinduzi katika
muziki wa dansi nchini.
“Katika
video hii nimeamua kwenda kurekodi nchini Afrika Kusini nikiwa na imani kwamba,
hata muziki wa dansi tunaweza kuleta mageuzi kwa kuingia gharama...Kwanini
wasanii wa muziki wa kizazi kipya waweze kutoka nje na sisi tusiweze, hapa mimi
nimewadhihirishia kwamba tunaweza,” alisema Bella na kuongeza kuwa video hiyo
imegharimu zaidi ya sh. milioni 17.
Aidha,
alibainisha kuwa jambo kubwa lililomfanya aende kurekodi video hiyo nchini humo
ni kutafuta soko la nje, kwa sababu watayarishaji wa muziki wa nje hasa Afrika
Kusini, wana uhusiano mzuri na watangazaji na watayarishaji wa vipindi vya
televisheni kubwa kama Channel O, MTV na
nyinginezo, hivyo inakuwa rahisi kwao kuipenyeza albamu ya mwanamuziki
waliyemrekodi.
0 Comments