Timu
ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer) inatarajiwa kuodoka
siku ya alhamisi kuelekea jijini Cairo nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa
marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa soka la ufukweni
utakaofanyika siku ya jumapili.
Tanzania
inapaswa kupata ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Misri utakaofanyika
siku ya jumapili jijini Cairo ili kufuzu kwa fainali za soka la ufukweni barani
Afrika zitakazofanyika visiwa vya Shelisheli kufuatia kupoteza mchezo wake
awali uliofanyika Escape 1 jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Msafara
wa timu ya Beach Soccer utakaoondoka na shirika la ndege la Ethiopia,
utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ahmed Msafiri Mgoyi, kocha mkuu John
Mwansasu, kocha msaidizi Ali Sheikh Alhashby, meneja Deogratius Baltazar na
daktari wa timu Dr Leonidas Rugambwa.
Wachezaji
ni Rajabu Chana Kipango, Ahmed Rajab Juma, Roland Revocatus Kessy, Samwel
Sarungi Opanga, Feisal Mohamed Ussi, Mohamed Makame Silima, Mwalimu Akida
Hamad, Juma Sultan Ibrahim, Kashiru Salum Said na Ally Rabby Abdallah.
TWIGA
STARS KUWAFUATA ZAMBIA IJUMAA
Msafara
wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars), unatarajiwa
kuondoka nchini siku ya ijumaa kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wake
wa kwanza dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia siku ya jumapili.
Twiga
Stars inaanzia hatua ya pili katika kuwania kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa
Wanawake baada ya kuwa katika nafasi za juu kwa viwango barani Afrika, na
endapo itafanikiwa kuwaondoa Wazambia itafuzu moja kwa moja kwa fainali hizo.
Msafara
utaongozwa na Blassy Kiondo (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji), Beatrice Mgaya
(kiongozi msaidizi), Rogasin Kaijage (kocha mkuu), Nasra Juma (kocha msaidizi),
Furaha Francis (Meneja), Christine Luambano (Daktari) na Mwanahamis Abdallah
(Mtunza vifaa).
Wachezaji
watakokweda Zambia ni Asha Rashid, Mwajuma Abdallah, Mwanahamis Omar, Donisi
Minja, Amina Bilal, Fatuma Bashiri, Esther Chabruma, Shelda Mafuru, Maimuna
Kaimu, Najiat Abbas, Stumai Abdalla, Fauma Issa, Thereza Yona, Fatuma Hassan,
Fatuma Omary, Sophia Mwasikili, Fatuma Khatibu na Etoe Mlenzi.
VPL
KUENDELEA KESHO
Ligi
Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea kesho (jumatano) kwa viwanja vitatu
kutimua vumbi, Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Young Aricans
watawakaribisha Kagera Sugar mchezo utakaoanza majira ya saa 10 kamili jioni.
Jijini
Tanga maafande wa Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Simba SC katika mchezo
utakaofanyika uwanja wa Mkwakwani, huku jijini Mbeya wenyeji Mbeya City
watawakaribisha timu ya ya Stand United kutoka mkoani Shinyanga kwenye uwanja
wa Sokoine.
YANGA,
PLATINUM ZAINGIZA MIL 91Mechi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africas dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbambwe iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam iliingiza mil 91,660,000 kutokana na watazamaji 14,563 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
Mgawanyo
wa mapato katika mchezo huo ni, VAT 18% sh. 13,982,033, Gharama ya tiketi sh.
12,380,000, Uwanja 15% sh. 9,794,694.92, Gharama za mchezo 15% sh.
9,794,694.92, TFF 5% sh. 3,264,898.31, CAF 5% sh. 3,264,898.31 na Young
Africans 60% sh.39.178,779.66
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 Comments