: Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) na wanachama wa Chama
cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno iliyofanyika katika viwanja vya Salender Bridge
Club jana jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliambatana na matembezi ya hiari
yalioyoanzia katika viwanja hivyo na kupitia Barabara ya Diomond Jubilee kabla
ya kurudi uwanjani hapo kupitia barabara ya AlhasanMwinyi na Kauli mbiu ya wiki
ya Afya ya Kinywa ni “Tabasamu la Maisha” Katikati ni Rais wa Chama Cha
Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro na wa mwisho
kulia ni Rais Mteule wa Chama hicho Dkt. Ambege Mwakatobe.
Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiangalia baadhi
ya machapisho yanayohusu Afya ya Kinywa na Meno kwenye banda lililowekwa katika
Viwanja vya Salender Bridge Club jana jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni
rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno. Kushoto ni
Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna
Carneiro.
: Baadhi ya Wanachama
wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) na baadhi ya wananchi
waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno
wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (hayupo pichani) jana jijini Dar es
Salaam.
(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI /WHVUM)
0 Comments