BURIANI AISHA MOHAMMED MBEGU (AISHA MADINDA)

NA KHADIJA KALILI
KATIKA maisha ya kila binaadamu  Mwenyeezi Mungu   amempangia kila mtu atapata riziki yake kwa njia fulani, wengine kutokana na njia ya kusoma sana  na wengine kisomo cha kawaida na cha kati huku wengine wakila kutokana na njia ya usanii iwe ni wa  maandishi, au vitendo.

Naam ndivyo ilivyokuwa kwa marehemu  Aisha Mohammed Mbegu   (Aisha Mandinda),   aliyekuwa mnenguaji tishio  na maarufu Tanzania nzima hilo halina ubishi  na alikuwa amejikita kwa staili ya kunengua ili  kupata kipato.

Katika enzi za uhai wake alikiri kwamba  alichagua kazi ya unenguaji, akafanikiwa na kudumu ndani ya kazi hiyo kwa takriban miaka kumi na sita,  binafsi yangu mimi nilipenda kumwangalia Aisha alivyokuwa Jukwaani akinengua huku akimwaga mikogo ambayo hakika mwenyewe alikuwa akisema hiki  ni kiuno cha Kigoma  kila alipokutana na mimi hivyo tulicheka na kugongeshana mikono.

Nilimfahamu  Aisha akiwa na kundi la Billbums ambalo lilikuwa likiundwa na yeye  pamoja na Mussa Hassan ‘Nyamwela’  walikuwa wakitoa burudani katika ukumbi wa Club Bilicanas miaka ya 1997-98 ndipo nilipomfahamu na kukubali kwamba alikua na kipaji cha kucheza.

Baada ya hapo nikaja  kumwona tena akiwa na bendi ya The African Stars  ‘Twanga Pepeta’ kazi yake ikawa ni ile ile ambako akiwa na bendi hiyo huku akiwa bado bint mrembo mwenye siha njema , shepu nzuri  halihkadhalika randi yake na wakati wote Aisha alipocheza alikuwa akimwaga tabasamu pana kwa mashabiki wake jambo ambalo lilimsababisha kupendwa sana  naha alipokosekana katika onyesho pengo lake lilionekana.

Jinsi nilivyomfahamu Aisha hakuwa na makuu  japo kuna wakati mungu alimjaalia akawa na maisha mazuri saana akajenga nyumba  tatu akawa na miliki na usafiri pia watoto wake aliweza kuwasomesha vizuri ikiwa ni pamoja na kwuapa chakula na malazi bora.

Lakini kuna siku nilishtuka na kupeleka hata kumsahau kutokana  na matumizi ya  dawa za kulevya  hakika sikuwa  na soni nilimkabili  na kumwomba azungumze wazi kwani atatoa somo kwa kina dada wengine ili wasijiingize katika matumizi ya dawa za kulevya.

Hakika hakuwa mbishi nilimuuliza mbona uko hivyo wakwetu kama jinsi tulivyokuwa na mazoea ya kuulizana kwa sababu ya wote kuwa na asili ya Mkoa wa Kigoma akawa anasita kidogo kuzungumza sababu nilimkuta katika ofisi za ASET , Kinondoni jijini Dar es Salaam akiwa na mazungumzo na Mkurugenzi wake wa zamani Asha  Baraka hivyo nikamuomba tuzungumze  yaliyomsibu.

Bila hiana alikubali hivyo tulikaa chemba tukazungumza nikampiga picha , kusema kweli hali yake  haikuwa mnzuri na hakuwa aisha yule ila kwa siku hiyo alizungumza vitu vya maana sana  kwamba anajutia kujiingiza huko jambo ambalo lilichangia kumuharibia maisha yake aliyoyatengeneza akiwa na nguvu zake kama vile kupoteza nyumba tatu alizokuwa amejenga.

Alisema kwa uchungu alighilibika na kujikuta akiuza nyumba zake sawa na bei ya kutoa bure kwa watu kutokanana  kukidhi kiu ya kupata fedha ili akanunue dawa za kulevya.

Nakumbuka baada ya kusema maneno hayo Aisha alilia nikambembeleza na kumwambia bado ana nguvu zake  asikate tamaa atapata tena bora alilie uzima wake tu akanisikiliza.

Tulizungumza mengi siku hiyo ambayo pia aliahidi kwamba amejipanga kurudi tena katika ulingo wa kunengua hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kupata raha zile alizokuwa akizitoa katika siku za nyuma.

Kama hiyo haitoshi hata Asha Baraka na yeye  akasema kwamba amedhamiria kumsaidia Aisha  ili aweze kurudi katika hali yake ya zamani hivyo  akawa anakwenda kuchukua fedha mara kwa mara kwa ajili ya manunuzi ya mahitaji yake  kama mwanamke wa mjini.

Nakumbuka pia mwaka jana kabla Club Bilicanas haijafungwa tulikutana na Aisha katika  onyesho la usiku wa Mwafrika hakika nikamsahau kwani alikuwa amependeza na amerudi katika  hali yake akanishtiua na kuniambia wakwetu upo nikamjibu hakyamungu umependeza hadi nimekusahau jamani  huku nikimsisitiza aendelee na tiba ya dawa za methodine ambazo alikua anatumia tukacheka kila mtu akaendelea na yake.

Wadau wa Twanga Pepeta wapania kumrudisha:
Hakika kupotea kwa kipaji cha Aisha kuliwauma wengi hili litabaki katika kumbukumbu zangu, nakumbuka mara kwa mara nilipopata fursa ya kukaa na wadau wa Twanga ambao hujitolea kwa hali na mali kama vile Fredito Mopao, yeye alikuwa mstari wa mbele kumrudisha Aisha katika hali yake ya kisaa.

Mara kwa mara alipenda kuniambia Kalili lazima katika safu ya Twanga pale tumrudishe Aisha na alijitahidi kwa hali na mali na hata marehemu Aisha aliwahi kusema kwamba anashukuru kwa jitihada za wadau wa Twanga hasa Mopao na yeye akiahidi kutowaangusha.

Lakini haikuwa jinsi vile sisi binadamu tulivyopanga kwani mungu nayeye tayari alishapanga ya kwake na limetimia.

Nilivyopokea taarifa za msiba wa Aisha:
Ilikuwa muda wa  saa saba mchana hivi  ndipo nilipopokea simu kutoka Kigoma kwa Asha Baraka na moja kwa moja akaniuliza unataarifa za msiba wa Aisha Madinda? Nikauliza  kwa taharuki unasemaje akarudia hivyo hivyo na kuniambia

“Nimepigiwa simu  na Daktari mmoja wa Hospitali ya Mwananyamala kuwa ameuona mwili wa Aisha Madinda  lakini hajui lolote hivyo mimi nikmo uwanja wa ndenge narudi Dar tutaonana akakata simu” anasema Asha.

Ndipo nikapandisha mbio ngazi na moja kwa moja nikamfuata mfanyakazi mwenzangu Betty Kangonga nikampa hizo habari akaniambia kwa sauti ya chini Mpigie simu Mkuchu umwambie, Mkuchu ambaye  ni Mhariri wa habari za Michezo na Burudani  hivyo nikampigia ananiambie kuwa yeye yuko mapumziko nyumbani nimpigie Salum Mkandemba aliyemwachia dawati na wakati nikifanya hivyo Mkandemba akaingia ofisini nikamweleza  akanipa pole na kuniambia niandie haraka hiyo habari nikamwitikia na kufanya hivyo.

Sikuishia hapo ili kujiridhisha na kifo hicho nikampigia simu Luizer Mbutu akanithibitishia kuwa Aisha amefariki dunia  na alifia nyumbani kwao hivyo pale hospitalini alifikishwa akiwa ameshafariki  na sababu za kifo chake  hazijafahamika.


Historia ya maisha ya Aisha kwa ufupi:

Jina lake kamili anaitwa Aisha Mohammed  Mbegu. Alipoanza kukata nyonga, akafahamika zaidi kwa jina la Aisha Madinda.
Aisha alizaliwa mwaka 1980 katika Hospitali ya Ocean Road, jijini Dar.
Elimu:


Kutokana na wazazi wake kuhamishiwa Mkoani Mbeya kikazi, Aisha alilazimika kuanza masomo yake ya msingi katika Shule ya Msingi Kiganamo iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma hadi alipohitimu darasa la saba mwaka 1992.


Mwaka 1993 alihamishia makazi yake Kigoma Mjini  na kujiunga na Sekondari ya Katubuka  lakini hakufanikiwa kuhitimu masomo yake ya sekondari baada ya wazazi wake kushindwa kumlipia ada hivyo aliishia kidato cha pili tu.

 Aisha ahamia rasmi jijini Dar es Salaam
Baada ya kukatisha masomo akiwa kidato cha pili, mwaka 1994 alihamia jijini Dar es Salaam  na kuanza kazi ya usafi katika Kampuni iliyojulikana kama Dar Cleaner ambapo alifanya kazi hiyo katika majengo mbalimbali.

Atupa fagio , ajikita katika unenguaji
Msanii huyo alijiingiza rasmi kwenye unenguaji Mwaka 1996 baada ya prodyuza wa muziki aliyefahamika kwa jina moja la Maloni Linje  kumtonya kuwa Club Billicanas ilikuwa ikihitaji wanenguaji. Mwaka huohuo, ukumbi huo ulianzisha kundi la kunengua la Bill Bams, akaanza kuitumikia.
Atimkia Umangani
Mwaka 1999, mkali huyo  wa nyonga ambaye tayari alishakuwa tishio katika kukata nyonga jukwaani, alipata mchongo wa  kwenda kupiga kazi Uarabuni katika mji wa Muscat akiwa ameambatana na mcheza shoo mwenzake aliyekuwa swahiba wake  Halima White ambaye sasa ni marehemu pia  walipiga kazi kwa  takriban mwaka mmoja na  mwaka 2000 walirejea nchini .
Alipotua tu  alichukuliwa na bendi ya Borabora Sound ambayo aliitumikia kwa miezi sita kabla hajaachana nayo kisha akasafiri tena kwenda Bahrain, Uarabuni ambapo alipiga mzigo katika kumbi mbalimbali nchini humo kwa miezi mitatu.
 Aliporejea Dar kwa mara nyingine, alijiunga na Bendi ya Kilimanjaro Connection ambapo pia hakukaa sana. na  mwaka 2000 mwishoni akaachana nao na kufanya biashara zake ndogondogo.

Ajiangusha kwa Twanga Pepeta:
Mwaka 2001, mkali huyo wa kukata nyonga ndipo  alijpoiunga  rasmi na bendi ya T wanga Pepeta Hapo alipiga kazi ya unenguaji hadi mwaka 2011, mwishoni alipohamia Bendi ya Extra Bongo  huku tayari ameshakuwa mtumiaji wa  matumizi ya madawa ya kulevya hadi kufikia hatua ya kushindwa kunengua mapema mwaka huu. Hata hivyo, ameacha kutumia madawa hayo.

 Familia :
Aisha  ni mama wa watoto wawili  na pia ana mjukuu mmoja.hadi mauti yanamkuta alikuwa katika dozi ya kujinasua  na matumizi ya mihadarati na alikuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa..

Aliwahi kuokoka ili apone miguu:
Kila  binaadamu anapoumwa huhangaika huku na kule ili aweze kupata tiba ya ugonjwa unaomsumbua hivyo Aisha aliwahi kuokoka  na alithibitisha hilo na alifanya hivyo kwa kuamini kwamba matatizo yake yangemalizika ikiwa ni pamoja .

Wadau wamlilia:
Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, alisema "sijajua
kilichosababisha kifo chake ni nini, kwa sababu hadi jana (Jumanne)
alikuwa mzima kabisa lakini ghafla ninaambiwa amefariki dunia!
Imenishtua sana na hadi sasa nashindwa kuamini."


Asha alisema kama mnenguaji huyo angekuwa anaumwa asingeshangaa,
lakini alikuwa mzima na ghafla zikaja taarifa za kifo, jambo ambalo
limemfanya apigwe na butwaa na kushindwa kuamini kuwapo kwa tukio
hilo.


Mkurugenzi huyo alisema Aisha alirejea hivi karibuni kutoka Dubai
alikokuwa amekwenda kwa shughuli za kimuziki na kwamba alikuwa
hajajiunga na bendi yoyote hadi mauti inamkuta.


  kwani alikuwa akiumwa  naye  Luizer Mbutu , hapa nilipo natetemeka  kwa msiba huu  sababu nilikua na marehemu na leo (Juzi Jumatano ) ndiyo ilikua aanze  mazoezi na bendi ya  Twanga Pepeta kwa ajili ya maandalizi ya miaka 16 Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta pia ilikuwa  tuwe pamoja katika kipindi cha Friday Night Live cha kituo cha EATV “ anasema  Mbutu.

Kwa upande wake Super Nyamwela ambaye amewahi kuwa kiongozi wa shoo ya
bendi ya Twanga Pepeta, alisema alipigiwa simu kuwa Aisha amefariki
dunia na kwenda mara moja hospitalini hapo na kuwa miongoni mwa watu
walioshuhudia huduma za kumuhifadhi katika chumba cha maiti akiwa na
baadhi ya ndugu zake ambao hadi jana walikuwa hawajui ni nini
kimemuua.
kujishughulisha na kazi ya kuelimisha vijana kuachana na utumiaji wa
dawa za kulevya kwa miezi kadhaa kabla ya kwenda Dubai hadi aliporejea
hivi karibuni.

Chanzo cha kifo  chake hakijulikani:
Ilifahamika kwamba  Aisha Madinda amefariki dunia jana saa nne asubuhi akiwa njiani
kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, bado haijajulikana ugonjwa uliosababisha mauti kumkuta
Aisha hadi hapo mwili wa marehemu utakapofanyiwa uchunguzi, kwa mujibu
wa madaktari wa Mwananyamala.
 

Polisi watoa kauli :
Alipotafutwa na juzi  jioni kuzungumzia kifo hicho, Kamanda wa
Kanda ya Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura,
alithibitisha kutokea kwa kifo hicho . Wambura alisema: "Leo (jana) majira ya saa mbili Aisha Mohamed Mbegu
maarufu kama Aisha Madinda alikutwa na rafiki yake Samira Saleh akiwa
amelala usingizi mzito kibarazani nyumbani kwake Mabibo (nyumbani kwa
Samira)."


"Hawa ni marafiki na wamekuwa wakipitiana kwenda Mwananyamala kupata
dawa za kutibu athari za matumizi ya dawa za kulevya. Alijaribu
kumwamsha lakini hakuamka. Akawaita majirani wakambeba na kumkimbiza
Hospitali ya Mwananyamala.


"Alipopimwa na madaktari ilibainika kwamba alikuwa katika usingizi
mzito ambao asingeweza kuamka tena kwa maana alikuwa ameshafariki
dunia," alisema zaidi Wambura.


Alisema tayari wameshafungua jalada la uchunguzi wa kifo na mwili wa
marehemu unatarajiwa kufanyiwa vipimo na madaktari wa
hospitali hiyo chini ya usimamizi wa Jeshi la Polisi baada ya ndugu wa
marehemu kuhusishwa.

Kauli ya Samira:
Samira huku akibubujikwa na machozi aliliambia gazeti hili, "asubuhi
nilipotoka ndani nilimkuta kalala kibarazani usingizi mzito,
nipojaribu kumwamsha hakuamka, ndipo nilipowatafuta majirani
wakanisaidia tukamkimbiza hospitali, lakini ndo hivyo tena tukaambiwa
amefariki."

Kauli ya mwisho ya Aisha kwa mwanawe
Mtoto wa marehemu, Naomi Omar jana aliliambia gazeti hili kuwa mama
yake Aisha, aliondoka nyumbani Kigamboni siku ya Jumatatu na kuaga
kwenda kwa rafiki yake Samira anayeishi Mabibo, Ubungo jijini Dar es
Salaam.

Naomi huku akibubujikwa na machozi kwa kumpoteza mamaye, anasema
Jumanne saa moja usiku alimpigia simu kumjulia hali na kumuuliza "Mama
mbona kimya, utarudi nyumbani lini? Aisha alimjibu
"nipo njiani ninakuja".

Kwa upande wake Super Nyamwela ambaye amewahi kuwa kiongozi wa shoo ya
bendi ya Twanga Pepeta, alisema alipigiwa simu kuwa Aisha amefariki
dunia na kwenda mara moja hospitalini hapo na kuwa miongoni mwa watu
walioshuhudia huduma za kumuhifadhi katika chumba cha maiti akiwa na
baadhi ya ndugu zake ambao hadi jana walikuwa hawajui ni nini
kimemuua.

Enzi za uhai wake Aisha amewahi kutamba kwenye bendi ya Twanga Pepeta
kwa muda mrefu kabla ya kusumbuliwa na miguu hali ambayo ilisababisha
ashindwe kufanya shughuli za muziki.

Hata hivyo, alitibiwa na kurudi jukwaani, lakini baadaye akaacha tena
kufanya shughuli za muziki hadi alipoibukia kwenye bendi ya Extra
Bongo inayoongozwa na Ally Choki.


Marehemu Aisha ambaye ameacha watoto wawili na mjukuu mmoja, Saidi Mbegu na
Naomi Omari, hakudumu sana Extra Bongo, kwani aliachana nayo na kuamua
kujishughulisha na kazi ya kuelimisha vijana kuachana na utumiaji wa
dawa za kulevya kwa miezi kadhaa .

Post a Comment

0 Comments