ALIYEKUWA
mnenguaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi
nchini Aisha Mohammed Mbegu
almaarufu kwa jina la Aisha Madinda pichani kulia amefariki dunia leo nyumbani kwao Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
kwa njia ya simu Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta Luizer
Mbutu alikiri kuwa Aisha amefariki dunia
na alifia nyumbani kwao sababu za kifo cheke bado hazijafahamika.
“Akizungumza
kwa masikitiko Mbutu alisema kwamba mwili wa merehemu tayari umehifadhiwa katika
Hospitali ya Mwananyamala “.
“Hapa nilipo
natetemeka kwa msiba huu sababu marehemu alikuwa mzima na leo ndiyo
ilikuwa aanze mazoezi na bendi ya Twanga Pepeta kwa ajili ya maandalizi ya
onyesho la maadhimisho ya miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta”
alisema Luizer.
Aliongeza
kwa kusema kwamba hapa natetemeka
siamini lakini tumepata nafasi ya kuingia katika chumba cha maiti na mwili nimeuona ni kweli Aisha amefariki na amefikishwa
hapa hospitalini akiwa tayari amefariki.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka ndiye
aliyekuwa wa kwanza kutoa taarifa za msiba huu wa Aisha baada ya kumpigia simu mwandishi wa
habari hizi akiuliza kama tayari nimepata taarifa ya msiba huo.
Msiba uko
Kigamboni maeneo ya Mikadi Beach ambako mipango ya mazishi inaendelea.
Kipaji cha Aisha Madinda kilivumbuliwa wakati akiwa na kundio la Bill Bums lililokuwa likitoa shoo kali ndani ya ukumbi wa Club Bilicanas Jijini Dar es Salaam.
0 Comments