TAMASHA LA MAGARI (AUTOFEST) KURINDIMA KWA SIKU TATU



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Dar es Salaam.
Masupa staa wa Tanzania wathibitisha ushiriki wao katika “Celebrities  Charity Car Wash” litakalo fanyika sambamba na tamasha la Auto Fest 2014. Linatarajiwa kufanyika tarehe 20th September, 2014 katika viwanja vya Biafra Kinondoni, Dar es Salaam.

Waliosibitisha ushirki wao ni Irene Uwoya,Odama, Kajala Masanja, Monalisa, Aunty Ezekiel, Lulu Michael, Johari, JB, Ritchie.

Tamasha hili kwa mwaka huu litajumuisha “Celebrity Charity Car Wash” ikiwa ni njia moja wapo yakutoa hamasa kwa wananchi kuchangia wahanga wa ajali nchini. “Kutokana na matukio mengi ya ajali nchini tumeona nakutambua kuwa wengi wa majeruhi hutibiwa bure basi ni vyema tukaandaa tukio linalo husiana na tamasha letu wakati huo huo tukiweza kuchangia mahitaji muhimu katika wodi hizi”.  Alisema Ally Nchahaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investments. “Tunarajia watu watahamisika kukemea madereva wanao tumia barabara vibaya tukielekea katika wiki ya usalama barabarani.

Tukio hili linalenga kuchangisha fedha kwa mfumo wa kuosha magari kwa bei yakuafikiana na Supa staa “CELEBRITY”.  Tunakaribisha watanzania kujitokeza kwa wingi katika uchangiaji huu. Lengo letu kwa mwaka huu likiwa nikuchangia Wodi ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Emergence Medicine Unit). 

Burudani kwenye tukio zitahusisha,  Gari lililo pambwa (Pimped) ambayo ni nafasi kwa wapenzi wa magari kuonyesha walivyoyapamba magari yao, Bingwa wa misele, Bingwa wa 4x4, B-Boy Dance, ‘Kids Car Zone,’ ambayo itawaburudisha watoto wa umri kati ya miaka mitano na 14 kwa program za magari na elimu muhimu ya magari na usalama barabarani, na kuweza kuburudika na mbinu mbalimbali za kuchezesha magari kama norinda “misele”.

Tamasha la Autofest mwisho wa wiki linategemea kuvutia watu wengi, na kulifanya kuwa tamasha kubwa na maarufu la magari Tanzania likiwa katika mwaka wake wa saba.

Kushiriki katika maonyesho ya mwaka huu tembelea mtandao wa www.autofest.co.tz.

 Kuhusu Vision Investments

 Vision Investments ni kampuni yawatanzania. Malengo ya Vision ni kutambua, kuunda, kuendeleza, kutoa na kuuza masuluhisho yanayofaa kukidhi mahitaji ya mteja ili kuhakikisha ufanisi wa hali ya juu, uwezo na thamani. Vision pia ni wataalamu wa, ushauri wa Masoko na usimamizi wa matukio.

 Kwa taarifa zaidi, tembelea: www.vision.co.tz

Post a Comment

0 Comments