IKIWA ni chache
tu kupita tangu aliyekuwa Rais wa Bongo Movie Steve Mengele ‘ Steve Nyerere’
kutangaza kung’atuka kwenye wadhifa huo ,Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF),Simon
Mwakifwamba amemuunga mkono kwa uamuzi huo.
Mwakifwamba
akizungumza na Tanzania Daima jana alisemas kwamba uamuzi wa Steve ni wa
busara na anapaswa kupongezwa hadi hapo
alipowafikisha Bongomovie inatosha.
“Binafsi
mwishoni mwa wiki nilikiwa miongoni mwa watu waliomshauri afanye hivyo kwani
hiyo ndiyo Bongomovie ambayo inatawaliwa na majungu kwakila kiongozi” alisema
Mwakifwamba .
“Mimi
nilimwambia steve Ijumaa iliyopita kwamba unaweza kulijenga jina lako kwa miaka
15 lakini ikifika mahali unaona majungu yamezidi na ili kuachana nayo bwaga
manyanga waachie Bongomovie yao hao wanaoona ni rahisi kuongoza ili waone kama
uongozi ni lelemama” alisema.
Steve Nyerere alitangaza kujiuzulu wadhifa huo
Ijumaa iliyopita kutokana na
kukithiri kwa majungu ndani ya
klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kutoaminiana kwa hali na mali.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam Nyerere ambaye
ni msanii wa kucheza filamu pia mbobevu katika kuchekesha hasa kwenye
kuiigiza sauti ya hayati baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania hayati Julius Nyerere ambako ndiko kuliko mpa
umaarufu huo hadi hivi sasa.
“Kikubwa
kilichonifanya nikimbie uongozi huu ni
kutokana na mlolongo wa migogoro kila
kunapokucha, kwani imekuwa ni kama jambo la kawaida kwa wasanii wa Bongomovie
kila mara baada ya kumalizika shughuli fulani kama misiba , mkialikwa
mahali hata kwenye khitma za kuwaombea
marehemu wao wameeka mbele fedha utasikia kala Nyerere kala hela nimechoka.
Hivi ni kiongozi gani ambaye atavumilia
kuzushiwa kashafa kila kunapokucha huku kwa silimia kubwa zikiwa ni za uongo
hasa la kusingiziwa kula fedha tuhuma ambazo hazina ukweli ndani yake” alisema
Steve kwa masikitiko.
Aidha
aliendelea kwa kusema kuwa anaona kama vile wasanii wenzake wanamtumia na
kumwona kama jalala la kutupa lawama zao ambazo hazina tija hivyo kwa kulinda heshima yake ambayo
amaeitengeneza kwa muda mrefu na kulinda heshima ya marafiki zake na viongozi ambao wamekuwa wakimsapoti kila
kunapokucha katika kulisukuma gurudumu la maendeleo ya wasanii ameamua kuachia
ili mwenye uwezo aje ashike usukani wake.
“Haya ni
maisha rafikiangu kwanini tugombee fito
ilhali wote lengo ni moja tu kujenga sanaa ambayo imetoa ajira kwa vijana wengi
nchini, mimi ni baba wa familia hivyo nimechoka kuona kila siku nakashifika
bila sababu za msingi acha sasa nikihangaika nitakachokipata nitagawana na
familia yangu mke wangu na watoto wangu na watu wengine ambao watakuwa
wakihitaji msaada wangu ”alisema Nyerere.
Uamuzi wa
Nyerere kubwaga manyanga Bongomovie umekuja siku chache baada ya kufanikisha
uzinduzi wa filamu ya ‘Mateso yangu
ughaibuni’ iliyorekodiwa nchini
Uingereza na kusimamiwa na Kampuni ya
Didas Entertainment.
“Nimefikia
uamuzi huu kwa roho safi wasije kuniua na presha za hovyohovyo hivyo maisha
yangu yataendelea nje ya Bongomovie na cheo cha Urais” anamalizia.
Nyerere
aliingia madarakani kwa kishindo mapema mwaka huu katika uchaguzi uliofanyika
kwenye ukumbi wa Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.
0 Comments