Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatarajia kufunga mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara.
Hafla
ya kufunga mafunzo hayo itafanyika kesho (Septemba 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi
kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Mafunzo
hayo ya siku tano yalishirikisha viongozi 34 wakiwemo baadhi ya waandishi wa
habari na Meneja wa Twiga Stars, na yaliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Henry Tandau.
0 Comments