Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, mkurugenzi
wa bendi hiyo Daniel Denga alisema kuwa ulizinduzi huo unafanyika baada ya
kuikarabati mpya ikiwa ina sura mpya zikiwamo za akina Adolf Mbinga ambaye
anajulikana sana kwa kibao chake cha Neema alichotunga akiwa na kundi la
Diamond Sound.
Mbali na Mbinga wanamuziki wengine mahiri waliotua katika kundi
hilo ni pamoja na Karama Legesu, Eddo Sanga, Shabani Lendi na Hamza Waninga.
Mbinga ametunga vibao vya Safari ya Victoria na kile cha Uke
Wenzake, ambavyo ni moto wa kuotea mbali.
Tayari kundi hilo limerekodi vibao vinne, ambavyo ni pamoja na
Uonevu, Tizama Mbele, Jojoo na Mke Mwenza.
Awali kundi hilo liliibuka upya mwaka 2012 lilipokuwa chini ya
Prince Muumin Mwinjuma kabla ya kuwa chini ya Waziri Sonyo na sasa linaongozwa
na Jonas Mnembuka anayesaidiwa na Mbinga ambaye pia ndiye kiongozi wa jukwaa.
Denga alisema kuwa wameamua kulisuka upya kundi hilo baada ya lile
la awali lililokuwa likiongoza na Prince Muumin Mwinjuma kushindwa kung’ara licha ya kupewa kila kitu.
0 Comments