Mashabiki waliojitokeza licha ya kupata burudani ya kandanda pia walipata ngoma ya asili.
Meza kuu.
Mahsbiki wakipagawa na mechi.
Hii ndiyo Bajaj iliyotolewa na Kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi kama zawadi kubwa kwenye michuano hiyo.
Mashabiki wakiwa wamejaa kwenye uwanja wakishuhudia mpambano huo.
David Albert kutoka Kituo cha Alliance na kupata sh . 200,000 huku timu ya Kata ya Mahina FC ikipata ikiibuka kuwa timu bora na yenye nidhamu na kuondoka na zawadi y ash. 200,000.
Paulo Godfrey akiwa na bao nane alijinyakulia kiatu cha dhahabu na fedha kiasi cha sh.200,000.
Washindi wa Pili wakipokea zawadi yao ya Kombe na fedha.
Hapa ikining'inizwa funguo ya Bajaj ambayo imekwenda kwa washindi wa michuano hiyo.
Bingwa Mkolani FC akipokea Kombe la ushindi wa michuano hiyo ya Pepsi Meyas Cup Mwanza.
Wachezaji wa Mkolani FC wakishangilia ubingwa huku wakinyanyua Kombe la ushindi.
TIMU ya Kata ya Mkolani FC imeibuka Mabingwa wapya wa Kombe la Meya 2014 baada ya kuichapa timu ya Kata ya Mirongo bao 2-1 jumamosi iliyopita katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Awali
katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ulioanza mapema saa 8:00 mchana kwa
timu ya Sokoni FC kuichapa Mnadani FC bao 3-0 na kuibuka mshindi wa tatu wa
michuano hiyo huku magoli ya Sokoni yakifungwa na Joseph Mwajalila dakika 33
kwa penati na Salimu Hamis dakika 39, 51na kuwapa tiketi ya ushindi wa tatu.
Akizungumza
na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu Mratibu wa michuano hiyo Paul Mganga
alisema fainali hiyo iliyoshuhudiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
Mhandisi Evarist Ndikilo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TFF Selestine
Mwesigwa, muasisi wa mashindano hayo Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza, Stanclaus
Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, Mwenyekiti wa Chama cha soka
Mkoa wa Mwanza (MZDFA), Jackson Songola na Katibu wa MZDFA, Nasibu Mabrouk.
Ndikilo
alisema mashindano hayo yamewawezesha vijana kuonyesha vipaji vyao, hivyo ni
vyema sasa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakawatumia vijana walionesha uwezo
kuunda timu ya Mwanza City FC kama ilivyofanya Jiji la Mbeya.
“Ni
bora mkaunda timu ya Mwanza City FC ili kushiriki ligi na huenda ikatinga ligi
kuu Bara kama walivyofanya wenzetu wa Mbeya na sasa timu ya Mbeya City FC
inashiriki ligi kuu, kwani timu zetu kongwe katika Mkoa huu za Toto FC na Pamba
FC zimeonekana kuishiwa mbinu za kuwawezesha kurudi ligi kuu,”alisema.
Mganga
alisema kwamba mchezo huo mkali ulikuwa ni wa vuta ni kuvute mashabiki walishuhudia timu
hizo zikienda mapumziko huku zikiwa
hazijafungana na katika kipindi cha pili
mchezaji Siraji Juma aliwainua mashabiki kwa kuandika bao la kwanza na bao la
pili likifungwa na Paulo Godfrey huku katika hekaheka ya kuokoa mpira
ulioelekezwa langoni mwake akijikuta akijifunga na hadi mwisho wa mchezo wadau
wa michezo walishuhudia timu ya Mkolani ikitawazwa kuwa mabingwa kwa kuinyuka
Mirongo FC bao 2 - 1.
Mashindano
hayo ya kombe la Meya 2014 yaliyodhaminiwa na Kampuni ya kutengeneza vinywaji
baridi vya Pepsi (SBC), Ndikilo ndiye aliekabidhi
zawadi ya kombe, fedha taslimu kiasi cha
Sh. Ml.1.5, medali ya dhahabu na Bajaj
ya mizigo yenye thamani ya Sh milioni 4.5, mshindi wa pili alinyakuwa Sh
milioni 2, kombe dogo na medali ya fedha.
Timu
ya Sokoni FC iliyoibuka mshindi wa tatu ilijinyakulia fedha taslimu Sh.Mil 1,
medali ya shaba na kombe dogo, aidha mfungaji bora Paulo Godfrey akiwa na bao nane
alijinyakulia kiatu cha dhahabu na fedha
kiasi cha sh.200,000.
Aidha
zawadi ya mwamuzi bora ilikwenda kwa David Albert kutoka Kituo cha
Alliance na kupata sh . 200,000 huku
timu ya Kata ya Mahina FC ikipata ikiibuka kuwa timu bora na yenye nidhamu na
kuondoka na zawadi y ash. 200,000.
0 Comments