MAKUBWA HAYA : WASTARA AOLEWA NA MWANAUME ASIYEMJUA



 
HiSTORIA KWA UFUPI
Wastara alizaliwa mwaka 1983 katika Hospitali ya Turiani iliyopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro akiwa ni mtoto wa tano kati ya saba waliozaliwa katika familia yao.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Wastara Juma.
Alisoma Shule ya Msingi Mvomero na baada ya kuhitimu darasa la saba alijiunga na masomo ya sekondari katika Shule ya Sekondari Kibamba Agriculture ambapo alipofika kidato cha pili aliacha shule.
MATUKIO YA UTOTONI
Mwandishi: Unakumbuka utotoni mwako ni matukio gani ya hatari ambayo ulikuwa ukiyafanya?
“Nilikuwa naparamia miti ya miembe, mikorosho kama sina akili nzuri huko nilikuwa nafuata pia ngedere kwani nilikuwa nawapenda sana, nakumbuka nilishawahi kuvunjika miguu yote pia kuvunjika mkono wa kulia kwa kuparamia miti.”
SABABU ZA KUACHA SHULE

Mwandishi: Umesema uliacha shule ukiwa kidato cha pili, nini sababu?
“Niliacha shule baada ya rafiki yangu kuiba hela nyumbani kwao ambapo alikuwa anakuja nazo shuleni tunakula wote chips,
wazazi wake walipogundua wakaja kushtaki shuleni nikawa natafutwa ili nisimamishwe mbele ya wanafunzi wote nieleze na kuchapwa, nilipogundua hivyo sikwenda tena shuleni maana nilikuwa nina aibu sana.”
AUZA MADUKA
Mwandishi: Je, baada ya kuacha shule ulienda wapi?
“Mama yangu alikuwa mfanyabiashara, alikuwa na duka la nguo na lingine la kuuza madini hivyo nilienda kumsaidia kwenye maduka hayo.”
Mwandishi: Ulifanya hizo biashara kwa muda gani?
APATA MCHUMBA
“Nilifanya kwa muda wa miezi mitatu nikapatiwa mchumba nikaolewa japokuwa nilikuwa simpendi.’’
Mwandishi: Sasa ilikuwaje ukaolewa na mwanaume usiyempenda?
“Nakumbuka nilikuwa na miaka kumi na sita na sikuwahi hata kumuona wala kuzungumza na huyo mwanaume kabla ya ndoa,
alienda moja kwa moja kwa mama yangu wakakubaliana na wakati huo wazazi wakishaamua huwezi kupinga ,hivyo nililazimika kuolewa hivyohivyo kwani mama yangu alikuwa akiogopa aibu ya kuzalia nyumbani kwa vile kwa mila zetu sisi Waarabu ukiwa na miaka hiyo msichana unaonekana ni mkubwa na unastahili kuolewa.”(Wastara baba yake alikuwa Mwaarabu.)
MUME AMZIDI UMRI
Mwandishi: Huyo mwanaume wako mlikuwa mnalingana naye umri au alikuzidi?
“Mwanaume alikuwa mkubwa sana kwangu hivyo kutokana na udogo niliokuwa nao sikuwa najua nini maana ya ndoa kitu nilichokuwa najua kufanya ni usafi tu, suala la mapenzi ndiyo lilikuwa ni shughuli haswa kwani nilikuwa sijui.”
TENDO LA NDOA
Mwandishi: Sasa mumeo alipokuwa akitaka haki ya ndoa ulikuwa unafanyaje?
“Ilikuwa ni kama tunapigana wakati huo ukifika na nilipopata ujauzito sikutaka hata aniguse hivyo mpaka mtoto anazaliwa sikushiriki tena tendo la ndoa na huyo mwanaume kwani nilikuwa namwambia kwamba naumia.”
MAISHA MAGUMU
Mwandishi: Vipi sasa maisha ya ndoa yalikuwaje?
“Maisha yalikuwa magumu sana kwani mwanaume aliyenioa hakuwa na kazi ya aina yoyote na mama hakuligundua hilo, baada ya kunioa alikuwa anaenda kushinda nyumbani kwao ndiyo ndugu zake wakawa wanatupatia chakula na kutulipia kodi.
“Baada ya kuwa na ujauzito wazazi wake walinichukua, nikaenda kukaa nao Zanzibar lakini nikawa nateseka sana ambapo mama yangu aligundua na kusema nije Dar kwani anataka kuniona na kipindi hicho alikuwa anaumwa, nilikuja kwa mama aliponiona alihuzunika sana kwani nilikuwa nimedho

Post a Comment

0 Comments