MSANII anyetamba kwa nyimbo za asili nchini Costa Siboka ‘Mfalme’ au unaweza kumwita ‘Mwana Ukerewe’ anatarajia kupamba katika onyesho la kumtafuta Miss Mwanza 2014.Akizungumza katika ofisi za Tanzania Daima jana Siboka alisema shindano hilo limepangwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu kwenye ukumbiulioko katika hoteli ya nyota tano ya Gold Crest.
“Katika shindano hilo nitaonyesha shoo yangu mpya inayokwenda kwa jina la ‘Engele yange’ maana yake ni samaki wangu ambao nimeuimba katika lugha ya Kikerewe” alisema.
Kadhalika
ameweka vionjo vya lugha ya Kisukuma ‘Nakutogile’ likiwa na maana ya Nakupenda.
Aidha pia
ametunga wimbo wa Kihaya ambao unakwenda kwa jina la ‘Otandekela Bojo ‘ (Usiniache).
Vile vile
anao wimbo mwingine aliouimba katika lugha ya Kikurya ‘Omuisike’ (Binti ambaye
bado hajaolewa ama mwali).
Siboka
ametamba na nyimbo za ‘Niwewange’ (wewe ni wangu ) ambapo alipiga katika mtindo
wa ‘Wawawa’, ‘Ndelule’ ambayo ni lugha ya Kinyamwezi huchezwa katika msimu wa
mavuno napia huimbwa kwa mashujaa wa uwindaji wanaporudi kutoka porini.
Pia Siboka
aliwahi kutwaa taji la watunisha misuli wa Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa
ujumla na kuiwakilisha nchi katika michuano ya Afrika iliyofanyika nchini Misri
ambako alitunukiwa Diploma ya kutunisha misuli na Rais wa Africa Body Building
Federation (AFBB).
Baada ya
hapo Siboka ataendela na ziara ya kutambulisha nyimbo zake mpya katika ziara ya mikoa ya kanda ya ziwa iliyodhaminiwa na
kinywaji cha wakulima Balimi Extra Lager na Kampuni ya CXC Africa.
0 Comments