ALI KIBA:KITI CHANGU KIPO ILA KINAVUMBI TU


MWANAMUZIKI Nyota nchini Ali Kiba pichani juu amesema kwamba licha kuwa amekuwa nje ya ulingo wa muzikikwa muda mrefu lakini hakuna mwanamuziki yeyote aliyewahi kushika nafasi yake.Hii ni kufuatia maneno ya mitaani kwamba amefulia na kwamba kuna msanii ambaye amechukua namba yake huku yeye akiwa amebakia stori tu za mtaani 'Zilipendwa'
Kiba alisema hayo katika mahojiano yake yaliyofanyika katika kipindi cha Spora Show kinachorushwa na kituo cha tv cha Clouds FM cha jijini Dar es Salaam.
Kiba ambaye alijibu swali hilo kwa kujiamini kwamba kiti chake kipo ila kina vumbi tu hivyo kazi anayotakiwa yeye ni kufuta vumbi na kuendelea kukaa na kama yupo msanii mwingine basi amekalia siti ingine lakini siyo ile yak wake.

Licha ya kuwa katika mahojiano hayo  Mtangazaji Spora alikuwa akimlazimisha Kiba akiri kama alikuwa na bifu na Msanii anayewika kwa sasa katika muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond’ hakuweka wazi kukubali ama kukataa kama wana bifu.
Kikubwa Kiba al;isimamia katika kile alichoamini kwamba yeye bado ni mwanamuziki mzuri huku akiahidi kurudi tena katika gemu kutokana na maombi mengi ya mashabiki huku akiwa anaahidi kuja na   mambo mapya yatakayokonga nyoyo zao  ipasavyo.
Aidha amesema kwamba trayari  yeye na mdogo wake Abdul Kiba wameshatengeneza kibao kipya kitakachokwenda kwa jina la ‘Kiba Square’ ambacho ni moto wa kuotea mbali.

Post a Comment

0 Comments