Baadhi
ya washiriki wa mashindano ya resi za Ngalawa wakijiandaa tayari kwa
kuanza mashindano hayo katika shamra shamra za tamasha la 17 la ZIFF
2014 linaloendelea visiwani Zanzibar. Picha na Zainul Mzige.
**********************************************
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
NGALAWA
zote 11 zilizoingia majini kukamilisha mzunguko wa saa mbili wa resi za
ngalawa mjini Zanzibar zilimarisha mashamshamu hayo bila najali na timu
tatu zilipewa zawadi za ushindi.
Resi
za Ngalawa kama zinavyojulikana ni utamaduni halisi wa visiwa vya pemba
na Unguja na ni sehemu ya tamasha kubwa la filamu la kimataifa la
Zanzibar ambalo linaendelea visiwani hapa.
Kwa
wale waliozaliwa maeneo ya bara, resi hizi zilikuwa kivutio kikubwa
kwao kutokana na maandalizi yanayofanywa kabla ya kuingia majini na dau
kunyanuliwa.
Wakati
dau limenyanyuliwa, maji yamekuwa yakichotwa ama ndani ya Ngalawa au
nje katika bahari kumwagia tanga katika hali inayoelezwa kuliimarisha
katika ukinzani wa upepo.
“mbio
za Ngalawa ni kipimo kikubwa cha Uzanzibari wetu na kila mwaka ZIFF
huhitimisha utashi wake wa kuwa na tamasha la nchi za jahazi kwa kuwa na
mbio za ngalawa” alisema mshehereshaji Muslim Nassoro Abdalla katika
shamrashamra zilizofanyika ufukweni kandoani mwa hoteli ya Tembo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya ZIFF ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe.
Mahmoud Thabit Kombo (mwenye t-shirt ya njano) akupiliza Kipenga
kuashiria kuanza kwa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye fukwe za
Hoteli ya Tembo visiwani Zanzibar.
Muslim
ambaye alisema kwamba mwaka huu walitaka kuwa na mbio za timu 20
(ngalawa) walishindwa kuhitimisha ndoto hiyo kutokana na masuala nje ya
uwezo wa ZIFF.
0 Comments