Meya
wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akifurahia jambo na Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho (kulia) na
Diwani wa Viti maalum Ilala Mh.Batuli Mziya (katikati) wakati wa ziara
ya viongozi wa TACAIDS kata ya Gongolamboto.
Mmoja wa wanachama wa Asasi ya Vijana ya St. Camilus inayojihusisha na utoaji wa elimu kuhusu VVU na Ukimwi kwa vijana kupitia sanaa mbalimbali Bi. Aquila Mawenya akisoma taarifa ya utendaji kazi wa asasi hiyo kwa Mwenyekiti wa wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho alipokutana na wanachama wa Asasi hiyo Kiwalani jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho (katikati) akiwa na baadhi ya wanachama Asasi ya Vijana ya St. Camilus inayojihusisha na utoaji wa elimu kuhusu VVU na Ukimwi kwa vijana kupitia sanaa mbalimbali alipowatembela eneo la Kiwalani jijini Dar es salaam
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Terezia Mmbando (kulia) akitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU na Ukimwi katika jiji la Dar es salaam kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho alipotembelea maeneo mbalimbali ya jiji hilo kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo katika ziara yake ya siku nne.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw.
Raymond Mushi akitoa tathmini ya hali ya maambukizi ya VVU katika jiji
la Dar es salaam na hatua zinazochuliwa na serikali kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali kukabiliana na janga hilo mara baada ya kupokea ugeni
kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi.
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ambaye pia ni diwani wa kata ya Gongolamboto akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho kwa kuhusu hatua iliyofikiwa na mikakati ya manispaa ya Ilala katika kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Baadhi ya viongozi wa manispaa ya Ilala wakiongozwa na Meya wa Manispaa hiyo Mh. Jerry Silaa (katikati) wakiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho (wa tatu kutoka kulia) alipotembelea Kata ya Gongolamboto kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo katika ngazi ya kata.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na viongozi na wakazi wa kata ya Gongolamboto jijini Dar es salaam alipotembelea eneo hilo kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo katika ngazi ya kata.
Mmoja wa wanachama wa Asasi ya Vijana ya St. Camilus inayojihusisha na utoaji wa elimu kuhusu VVU na Ukimwi kwa vijana kupitia sanaa mbalimbali Bi. Aquila Mawenya akisoma taarifa ya utendaji kazi wa asasi hiyo kwa Mwenyekiti wa wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho alipokutana na wanachama wa Asasi hiyo Kiwalani jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho (katikati) akiwa na baadhi ya wanachama Asasi ya Vijana ya St. Camilus inayojihusisha na utoaji wa elimu kuhusu VVU na Ukimwi kwa vijana kupitia sanaa mbalimbali alipowatembela eneo la Kiwalani jijini Dar es salaam
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Terezia Mmbando (kulia) akitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU na Ukimwi katika jiji la Dar es salaam kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho alipotembelea maeneo mbalimbali ya jiji hilo kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo katika ziara yake ya siku nne.
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa ambaye pia ni diwani wa kata ya Gongolamboto akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho kwa kuhusu hatua iliyofikiwa na mikakati ya manispaa ya Ilala katika kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Baadhi ya viongozi wa manispaa ya Ilala wakiongozwa na Meya wa Manispaa hiyo Mh. Jerry Silaa (katikati) wakiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho (wa tatu kutoka kulia) alipotembelea Kata ya Gongolamboto kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo katika ngazi ya kata.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na viongozi na wakazi wa kata ya Gongolamboto jijini Dar es salaam alipotembelea eneo hilo kuangalia hatua zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo katika ngazi ya kata.
Katibu
wa mtandao wa Vikoba vya watu wanaoishi na VVU (IDINEPA VICOBA) kata ya
Kiwalani Bw. Shaban Mwasa Wamikole akimkabidhi risala ya kikundi hicho Mwenyekiti
wa wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho alipokutana
na wanachama wa kikundi hicho katika kata ya Kiwalani jijini Dar es
salaam.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
Licha
ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali za udhibiti wa maambukizi mapya
ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, Jiji la Dar es salaam limefanikiwa
kupunguza kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 9.8 za mwaka 2007/2008
hadi kufikia asilimia 6.9kutokana na jitihada zilizofanywa na serikali zikiwemo za uundaji wa kamati shirikishi za mkoa kudhibiti maambukizi hayo.
Hayo yamebainishwa katika
taarifa ya hali ya maambukizi ya VVU na Ukimwi iliyotolewa na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Terezia Mmbando kwa Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho
alipotembelea maeneo mbalimbali ya jiji hilo kuangalia hatua
zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo.
Akisoma
taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam Bi. Mmbando ameeleza kuwa janga
la Ukimwi ni tatizo la dunia nzima na limekuwa kikwazo cha maendeleo ya
jamii hapa nchini na kuongeza kuwa jitihada za kudhibiti maambukizi ya
Ukimwi jijini Dar es salaam zimechukuliwa kupunguza maambukizi ikiwa ni
pamoja na uanzishaji rasmi wa kamati za kuratibu na kusimamia shughuli
za kudhibiti Ukimwi kuanzia ngazi ya mkoa, halmashauri, ngazi ya kata na
mtaa.
Amesema jiji la Dar es salaam linakabiliwa na changamoto ya ongezeko la kubwa la watu ikilinganishwa na mikoa mingine
hali inayochangia mwingiliano wa tamaduni, shughulim mbalimbali,
masuala ya kijamii,kimila na kiuchumi na kuongeza kuwa kwa mujibu wa
Sensa ya Watu na Makazi 2012 idadi ya watu imefikia 4,364,54, wanaume wakiwa 2,125,786 na wanawake 2,238,755 sawa na ongezeko la asilimia 5 kwa mwaka.
Hali ya VVU na Ukimwi mkoa wa Dar es salaam.
Hali
ya maambukizi ya Ukimwi katika jiji la Dar es salaam kwa mujibu wa
matokeo ya utafiti uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuhusu
viashiria vya Ukimwi na Malaria mwaka 2011/2012 inaonesha kuwa kiwango
cha maambukizi ya VVU kitaifa ni wastani wa asilimia 5.1 ambapo
maambukizi kwa wanawake ni asilimia 6.2 na wanaume ni asilimia 3.8.
Sababu za maambukizi.
Miongoni
mwa sababu zinazochangia kuendelea kuwepo kwa maambukizi mapya ya VVU
katika mkoa wa Dar es salaam ni pamoja na kasi ya ukuaji wa jiji na
shughuli za kibiashara hali inayosababisha mwingiliano wa watu na
mahusiano ya kimapenzi pia baadhi ya wakazi kutobadili tabia licha ya
kupatiwa elimu ya kujikinga na maambukizi ya ya ugonjwa huo.
Sababu
nyingine ni hali ngumu ya uchumi hususani maeneo yenye mkusanyiko
mkubwa wa wakazi wa kipato cha chini,kuongezeka kwa vitendo vya ngono
isiyo salama hususani maeneo yenye nyumba nyingi za kulala wageni, kumbi
za starehe, madangulo na makundi yaliyo katika mazingira hatarishi ya
madereva wa magari ya masafa marefu.
Aidha, ngoma za usiku zinazokesha hasa maeneo ya pembezoni mwa jiji zinazoambatana na unywaji wa pombe kupita kiasi na
uwepo wa makundi maalum ya watu wanaofanya biashara ya ngono na wale
wanaotumia dawa za kulevya hali inayowafanya washindwe kutoa maamuzi
sahihi ya kujikinga na VVU ni miongoni mwa sababu zinazochangia
maambukizi mapya ya VVU.
Hatua zilizochukuliwa kudhibiti maambukizi.
Mkoa
kwa kushirikiana na halmashauri za manispaa na wadau mbalimbali pamoja
na mambo mengine umeendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya
kujikinga na maambukizi ya VVU,kuhamasisha upimaji wa hiari wa VVU pia
kuongeza nguvu katika mapambano ya kuzuia maabukizi kutoka mama kwenda
kwa mtoto kupitia kliniki za afya ya uzazi.
Hatua
nyingine ni utoaji wa huduma za tiba na virutubisho kwa wagonjwa,
kuwahudumia watoto yatima na wale wanaoishi mazingira hatarishi pia
kutoa mafunzo ya ujasiriamali na kuhamasisha uundaji wa vikundi vya
ujasiriamali kwa wanaoishi na VVU ili waweze kumudu gharama za maisha na
uundaji wa vikundi vya sanaa vya vijana kwa ajili ya kutoa elimu ya VVU
na Ukimwi kwa vijana walio katika mazingira hatarishi ya maambukizi
katika jiji la Dar es salaam.
0 Comments