Baadhi
ya watoto wa Shule za Msingi kutoka Wilaya ya Ilala wakionesha vipaji
vya kucheza ngoma wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya sanaa
yaliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata),na kufadhiliwa na
Kampuni ya Msama Promotions . Jumla ya watoto 200 wamenufaika na mafunzo
hayo.
Mmoja wa wanafunzi akionesha mitindo ya mavazi.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Buguruni Visiwi wakionesha mitindo mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza katika hafla ya
kufunga mafunzo ya sanaa kwa watoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Basata na kudhaminiwa na Kampuni ya Msama
Promotions. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza
na Ofisa Tawala wa Kampuni ya Msama Promotions, Hamis Mussa.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza akizungumza wakati wa hafla hiyo.
0 Comments