Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea moja ya kati ya mbili ya Kadi
za Chadema kutoka kwa aliekuwa Mwanachama wa Chadema,Mrisho Issa mkazi
wa Kijiji cha Msata,ndani ya Jimbo la Chalinze.Mwingine alierudisha kadi
ni Kassim Msakamali (hayupo pichani).
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (katikati) akiwainua mikono Wanachama
wapya wa Chama cha Mapinduzi,Kassim Msakamali (wa pili kushoto) na
Mrisho Issa (wa pili kulia) ambao wote ni Wananchi wa Kijiji cha
Msata,Chalinze.Kulia ni Meneja wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la
Chalinze (CCM),Steven Kazidi.
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete aiwasalimia wananchi wa
Lugoba,Chalinze.
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akiambatana na Mwenyekiti wa
Kampeni wa Chalinze (CCM),Saleh Mpwimbwi (kushoto) pamoja na Msafara
wake wakielekea kuhani Msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa
kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze
jana Machi 17,2014.
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete na ujumbe wake wakishiriki kwenye dua
ya pamoja mara baada ya kufanyika kwa kisomo cha kumuombea Marehemu
ambaye ni Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman (alieketi nyuma ya mgombe) mkazi
wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la
Chalinze jana Machi 17,2014
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (aliesimama kulia) akizungumza
machache wakati alipofika kuhani msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman
mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la
Chalinze jana Machi 17,2014.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
0 Comments