Floyd Mayweather Jr Mbabe anayetaraji kuhitimisha zama zake A. Kusini

Floyd Mayweather Jr Mbabe anayetaraji kuhitimisha zama zake A. Kusini


Floyd Mayweather Jr
Mbabe anayetaraji kuhitimisha zama zake A. Kusini
*Ni mwanamichezo anayeongoza kwa fedha, matumizi
LEO katika maisha ya wenzetu tutakuwa na mbabe Floyd Mayweather Jr ‘Money’ anayetokea katika ukoo wababe waliowahi kutikisa dunia kwa kutwaa ubingwa wa ngumi wa duniani ambao ni baba yake mkubwa Floyd Mayweather Sr na baba zake wadogo, Jeff Mayweather na Roger Mayweather.
Mbabe huyo ambaye ametangaza kwa mara nyingine kwamba anamipango ya kucheza pambano lake la mwisho Septemba 2015, nchini Afrika Kusini.
Bingwa huyo aliyabainisha hayo wakati alipokuwa nchini Afrika kusini katika ziara yake ya kutangaza mchezo huo nchini humo katika majimbo sita ikiwamo miji ya  Bloemfontein, East London na Cape Town.
Bondia huyo ambaye ni rafiki wa karibu wa rapper 50 Cent ana rekodi ya kushinda mara 45 na hajawahi kupigwa hata pambano moja tangu aanze mchezo huo mwaka 1996, huku akishinda kwa ‘KO’ (26). 
Ujio wa mwakani wa bondia huyo utakuwa wa pili baada ya ule wa kwanza ambao mbabe huyo alifanikiwa kupewa heshima ya kuwa mgeni rasmi wa utoaji wa tuzo wa mwanamichezo bora wa mwaka wa Afrika Kusini.
USICHOKIJUA
Floyd Mayweather amefuata nyayo za baba yake mzazi Floyd Mayweather aliyekuwa bingwa wa dunia, baba yake mdogo Jeff Mayweather alikuwa bingwa wa uzito wa juu wa IBO na baba yake mwingine, Roger Mayweather alikuwa bingwa wa dunia mara mbili, kabla ya kuacha na kuwa kocha wa kijana huyo.
Ngumi za ridhaa alizocheza takribani mapambano 84 yalimuwezesha Floyd, kung’aa na kuonesha kipaji chake kutokana na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa taifa nchini Marekani ‘National Golden Gloves’ kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 1993, hadi 1996.
Floyd kutokana na ugumu wake wa kutopigika, aliokuwa nao, wenzake walimpachika jina la utani ‘Bitch Boy’ kutoka na usugu wa uso wake, uliokuwa hauchubuki wala kuchanika akiwa ulingoni.
Sifa yake kubwa ni ukwepaji wa makonde akifananishwa na enzi za baba yake, Floyd Mayweather Sr na baba yake mdogo, Roger Mayweather, ambao ndio wamekuwa makocha wake.
Baba yake mdogo, Roger Mayweather alichukua jukumu la kumfundisha baada ya baba yake mzazi, Floyd Mayweather Sr. kuhukumiwa kifungo jela baada ya kukutwa na dawa za kulevya ndani ya gari lake mwaka 1993.
Baada ya Mayweather Sr. kutoka jela alimchukua tena mwanawe na kumuendeleza kumfundiusha na kumuwezesha kumshinda kwa KO, Sam Girard.
Mwaka 2006, akiwa na miaka 29 pekee, Mayweather aliviita vyombo vya habari na kuvieleza nia yake ya kutaka kustafu baada ya kucheza na Oscar De La Hoya.
Hatimaye Mei 5, 2007 pambano kati yake na bingwa wa WBC, Light Middle, De La Hoya na kufanikiwa kushinda lakini alibatilisha uamuzi wake wa kustaafu ngumi.
FEDHA
Floyd Mayweather anamiliki utajiri unaofikia kiasi cha dola milioni 216 (sawa na shilingi milioni 216).
MATUMIZI YA FEDHA
Mbabe huyo ambaye ndiye mwanamichezo anayelipwa zaidi amekuwa akielezwa kutumia fedha kwa fujo zaidi kuliko wanamichezo wengine, kwani hata katika pambano lake lililopita la Septemba alilpwa kiasi cha dola milioni  41.5. 
Kutokana na matumizi yake makubwa ya fedha mbabe huyo amepewa jina la utani la ‘Money’.
Tofauti na nyota wengine Mayweather amekuwa na mpambe anayebeba mikoba ya mamilioni ya fedha katika matumizi yake na kulipa kwa fedha taslim badala ya kulipa kwa hundi kama ilivyo kwa nyota wengine.
Hupendelea kuvaa viatu vya hali ya juu na hata nguo zake za ndani amekuwa akivaa mara moja na kutupa.
Wapambe wake na hata wafanyabiashara zake wamepewa jina la ‘The Money Team’ alilalamikiwa kutumia fedha vibaya kiasi cha kutokuwa na fedha benki hali iliyomfanya amuonesha mwandishi wa ESPN kitabu chake cha benki kilichokuwa na dola milioni 123 na kumwambia kwamba hiyo ni akaunti moja tu badoi nyingine.
Kwa kuonesha kwamba anatumia fedha kufuru mbabe huyo alipokuwa katika moja ya ziara yake nchini Marekani alikuwa akitumia ndege binafsi akiwa amempakia kinyozi wake pekee ingawa mara zote anakuwa amenyoa kipara huku wapambe wake wengine akiwa amewakodia ndege nyingine.
Akiwa jijini New York alitumia karibu dola 250,000 (shilingi miloni 400) kwa kununua vito vya mwanaye, Iyanna mwenye umri wa miaka 13 ambavyo ni Hereni na mikufu.
USAFIRI   
Hutumia kiasi kikubwa cha fedha katika ununuzi wa magari ambako anaelezwa amekuwa akinunua magari ya kifahari mawili mawili kwa rangi tofauti kwa nia ya kutumia katika majiji mbalimbali ya Marekani.
Inaelezwa kwamba kununua magari ya rangi tofauti yamekuwa yakimuwezesha kutambua jiji analokuwa amefika kwa mfano anapokuwa Las Vegas hutumia gari jeupe na anapokuwa Miami anatumia jeusi.
MAKAZI
Floyd Mayweather anaishi Las Vegas katika jumba ambalo alilinunua na kulikarabati kwa dola milioni 9. Jumba hilo lipo kwenye eneo lenye ukubwa wa futi za mraba 22,000. Vyumba vitano vya kulala, vyumba saba vya kuoga, baa ndogo, chumba cha kuonea sinema, ukumbi wa mikutano, eneo la kucheza gofu, gereji.
WASIFU
JINA: Floyd Mayweather Jr ‘Money’
UMRI: 37
KIMO: mita 1.73
UZITO: kilogramu 68
Makala hii imendaliwa na Shabani Matutu kwa msaada wa mashirika mbalimbali ya kimataifa
.DVD MPYA KUTOKA KWA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION AMBAZO ZINATARAJIWA KUWA HEWANI WIKI IJAYO NA MAPAMBANO YOTE YA NGUMI YATAKAYOFANYIKA WIKI IJAYO ZAIDI FIKA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO PIGA SIMU 0713406938

Post a Comment

0 Comments