Na Mwandishi Wetu
Rajabu Mhamila Super D' |
KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila Super D' anajivunia mafanikio yake katika mchezo
wa ngumi nchini baada ya mwanzoni mwa mwaka jana 2013 kufanya ziara ya mikoa 16 ya Tanzania bara
Aliyasema hayo wakati wa kufunga mashindano ya mchezo wa ngumi
yanayokwenda kwa jina la Nelson Mandela OpenChampion ship 'Unajua mimi
mwaka jana nilifanya ziara ya kuamasisha mchezo wa masumbwi nchini nikiwa
na lengo moja tu la ngumi zienee Tanzania nzima sasa naisi kazi
niliyofanya imefanikiwa kutokana na mashindano haya kuja kushiliki watu
wengi wa mikoani'
Super D ambaye katika kufuraishwa kwake
kwa vijana wengi waliojitokeza mikoani kuja kushiliki alitoa DVD za
Mafunzo ya mchezo wa masumbwi nchini kwa kila bondia aliyeshiliki kwa
ajili ya kwenda kujifunza mbinu mbalimbali
pamoja na baadhi yao kuwapatia flana
zenye nembo yake kama ishala ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi ambazo
amebuni mwenyewe zikiwa na mcholo wa Glove pamoja na mahandishi
yanayosomeka Super D Boxing Coach
aliongeza kwa kusema unajua mikoani kuna
vipaji vingi sana hata hivyo bado awajawezeshwa kwa kuwa kwanza
upatikanaji wa vifaa vya kufundishia ni tabu sana kwa watu wa mikoani
hivyo wakiwezeshwa au wadau mbalimbali wakijitokeza kuwekeza kwenye
mchezo huu unaweza ukapanda chati nchini
Super
D ambaye anajishughulisha na uhuzaji wa vifaa vya mchezo huo amekuwa
kiungo muhimu katika upatikanaji wa vifaa hivyo kwa mabondia na makocha
kwa wepesi wa hali ya juu na kuufanya mchezo wa ngumi uzidi kusonga
mbele kila kukicha nchini Tanzania
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
0 Comments