HAFLA YA UZINDUZI WA KITABU CHA SIMULIZI ZA MZEE MANDELA.

Ndugu zangu, 

Nami nitapata fursa ya kutoa hotuba. Nitazungumzia umuhimu wa kuhifadhi historia kwenye maandishi ili iwe ni kumbukumbu ya miaka mingi kwa wengine kujifunza. Maana, historia haibadiliki, lakini inapotea.
 
Na taifa linalodai kuwa watu wake wameelimika tunalipimaje?
Jibu; Ni kwa kuangalia idadi ya machapisho yanayozalishwa kila mwaka. Kuangalia pia ubora wa machapisho hayo.
 
Na machapisho ni jambo moja, na kuyasoma machapisho hayo ni jambo jingine kabisa.
Tuna lazima ya kuwajengea watu wetu kiu ya kupenda kusoma. Ni moja ya malengo yangu ya kuandika kitabu cha ' Simulizi Za Mzee Madiba'. Kwamba watu watafute vitabu zaidi vya kusoma. 

Leo Jumamosi pale Makumbusho ya Taifa nitasimulia utoto wangu na jinsi nilivyoanza kuelewa maana ya vita vya ukombozi kutoka Ubaguzi wa rangi Afrika Kusini kutokana na kucheza mpira na watoto wa wakimbizi wanachama wa ANC waliokuwa wakikaa jirani na sisi pale Biafra Kinondoni. 

Leo Jumamosi kutakuwa na nafasi pia ya kuulizana maswali, kujadiliana na kupeana ufafanuzi, kama Watanzania.

 Mgeni Rasmi Kwenye Uzinduzi Ni Ndugu Mobhare Matinyi.
Siku Njema.
Maggid Mjengwa 0754678252

Post a Comment

0 Comments