Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI
wa Viwanda Biashara na Masoko ambaye pia ndio mbunge wa Handeni, Dkt
Abdallah Kigoda, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la
Utamaduni, lililopangwa kufanyika Katika Uwanja wa Azimio, wilayani
Handeni mkoani Tanga, Desemba 14 mwaka huu.
Tamasha
hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani hapa, huku likitarajiwa
kuwa la aina yake kutokana na maandalizi yanayoendelea kushika kasi,
ambapo kwenye uwanja huo, Tamasha hilo litaanza saa 2 asubuhi hadi saa
12 za jioni.
Akizungumza
jana mjini Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema
maandalizi yamezidi kushika kasi kwa kuangalia mazoezi ya vikundi kadhaa
vitakavyotoa burudani katika tukio hilo.
“Tunashukuru
Mungu kuona mambo yanazidi kuwa mazuri kwa kuhakikisha kuwa Desemba 14
mwaka huu tunafanya tamasha lenye mguso na kila mmoja wetu kufaidishwa.
“Huu
ni wakati wa kila mtu kujipanga ili aje kushiriki kwa namna moja ama
nyingine, ukizingatia kuwa juhudi hizi zote zipo kwa ajili ya kujenga
ushirikiano kwa watu wote,” alisema Mbwana.
Wadhamini
katika tamasha hilo ni pamoja na gazeti la Mwananchi, Clouds Media
Group, ni Phed Trans, Clouds Media Group, Grace Products, Screen Masters
na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd,
Katomu Solar Specialist, PLAN B SOLUTIONS (T) LTD, Country
Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group duka la mavazi la Chichi
Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd,
ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’,
Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog, Pamoja Pure Blog na Taifa
Letu.com.
0 Comments