SERIKALI KUTUMIA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 219 KUJENGA GATI 4 KATIKA BANDARI YA MTWARA




Na Fatma Salum-Maelezo
Serikali kutumia takriban  dola za marekani milioni 219 kujenga  gati 4 katika bandari ya Mtwara ambapo tayari taarifa ya upembuzi yakinifu imekamilika.

Hayo yamesemwa  leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi Uwekezaji na Uwezeshaji  toka Ofisi ya Waziri Mkuu John Mboya wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Akieleza zaidi  John amesema mradi huo ni matokeo ya utekelezaji wa kanuni za Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ya mwaka 2011 ambapo sektabinafsi inahusikanakukarabati,kujenga,kuendesha,kutunza au kusimamia mradi mzima.

Akifafanua zaidi John amesema Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia idara yake imeendaa mafunzo kwa maofisa 60 walioteuliwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya DPP.

Akitolea mfano alisema Serikali inaweza kuwa na mkataba na muwekezaji katika mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa  km 100 wenye viwango Fulani ambapo muwekezaji atatakiwa kusanifu, kujenga na kuendesha kwa gharama zake na hatimaye baada ya kurudisha mtaji wake na faida,anakabidhi mradi huo serikalini.

Alitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa barabara ya Dar es salaam-chalinze (km 100)kuwa barabara ya haraka (Expressway)ambapo wakala wa barabara umekamilisha hatua za awali za upembuzi yakinifu wa awali.

Mradi mwingine ni ujenzi wa bandari mpya ya bagamoyo na eneo huru la biashara ambapo Serikali inashirikiana na mwekezaji kutoka China, ambapo majadiliano na mwekezaji yanaendelea ili mradi huu ulete tija kwa Taifa.

Post a Comment

0 Comments