MPANGO wa Taifa wa Damu Salama umevuka lengo la
makusanyo ya damu katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu kwa
kukusanya chupa za damu 38,948
ambazo ni asilimia 111 ikilinganishwa na chupa 36,278 zilizokusanywa kutoka
Januari hadi Machi mwaka huu.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mpango wa Damu Salama,
Bw. Rajab Mwenda akizungumza jana Dar es Salaam alisema kanda inayongoza kwa
uchangiaji ni Mashariki na Kanda ya Ziwa.
Alisema mafanikio hayo yametokana na uanzishajiwa
mpango wa damu salama wa kampeni ya kuhamasisha uchangiaji damu kwa
hiari katika jamii na
kushirikisha wadau.
Bw. Mwenda alisema maadhimisho ya siku ya
wachangia Damu duniani ambapo lengo la kukusanya chupa za Damu 8,500 kutoka kanda sita za mpango wa Taifa
wa damu salama liliwekwa na mpango ulifanikiwa kukusanya jumla ya chupa 8,683
Alisema
Mpango wa Damu salama kushirikiana na wadau mbalimbali kama asasi za kiraia nayo imeongeza makusanyo ya damu toka vituo
vidogo vya kuchangia damu Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma kutoka chupa za damu 2,560 mpaka chupa 3,151 kufikia Aprili hadi Juni mwaka huu.
Aliwaomba wadau kuendelea kuelimisha na
kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari kwa kutumia vyombo
vya habari, mitandao ya jamii na vipeperushi.
Bw. Mwenda
alisema ushirikiano ni mdogo
kati ya wahamasishaji wa Mpango wa damu
salama na viongozi wa Taasisi mbalimbali, matumizi mabaya ya damu kidogo
inayopatikana katika hospitali zetu na miundo mbinu hafifu hususan barabara
mbovu wakati wa ukusanyaji na usambazaji
wa damu.
Alisema
changamoto nyingine ni uuzwaji
wa chupa za damu kunakofanywa na baadhi ya watumishi wa hospital ambao si
waaminifu hivyo kukatisha tamaa wachangia damu kwa hiari.
Bw. Mwenda alisema Serikali
kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilianzisha Mpango wa Taifa wa Damu
Salama mwaka 2005 ili kuhakikisha uwepo wa damu salama na ya kutosha kwa wote
wanaohitaji.
Alisema
shughuli za mpango ni pamoja na uhamasishaji jamii kuhusu uchangiaji damu wa
hiari, ukusanyaji upimaji na usambazaji wa damu salama mahospitalini.
“Mpango
wa Taifa wa Damu salama unafanya kazi kwa kushirikianana kitengo cha kuzuia
magonjwa (CDC) na wadau wengine wa Chama
cha Msalaba Mwekundu na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)” alisema
Bw. Mwenda.
Alisema
Mpango wa Taifa wa Damu salama uliweka lengo la kupunguza maambukizi ya virusi
vya ukimwi (VVU) katika damu iliyokusanywa asilimia 1.1 kwa kipindi Aprili-
Juni ikilinganishwa na asilimia 1.2 kipindi cha Januari hadi Machi baada ya
kujikita katika suala la uhamasishaji na kutoa damu toka kwa jamii ambayo ni
salama, kuboresha dodoso la wachangiam damu na kuendelea kuelimisha jamii
kuhusu umuhimu wa kuchangia damu na wachangiaji kujiepusha na tabia hatarishi
ili wawe wachangiaji wa kujirudia.
0 Comments