KAMANDA na gwiji wa muziki wa dansi katika bendi ya Msondo
Maalim Muhidin Gurumo (73) ametangaza
kuacha rasmi kujighulisha muziki
wa dansi kama jinsi aliyoifanya kwa muda wa miaka 53.
Gurumo aliyasema hayo
leo saa sita mchana katika
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO Dar es Salaam.
“ Leo nimekuja kuwaga
rasmi wanamuziki na wapenda muziki na waliokuwa mashabiki wangu kwa ujumla , sitaki tena muziki ila ikumbukwe
kwamba muziki ni asili yangu ila
sasa nimeamua kustaafu kwa moyo
mmoja hivyo naahidi kuwa nitawasaidia
wanamuziki wanaobaki kwa uhuru na moyo mmoja” alisema Gurumo. ), jijini
Wakati huohuo, Gurumo anasema anastaafu akiwa hana kitu cha
maana katika tasnia ya muziki wa dansi licha ya kuutumikia na kufanya kazi kwa
moyo wake wote kwa kipindi cha miaka 53
iliyopita.
“Nilianza kuimba nikiwa
kijana wa umri wa miaka 20 mwaka
1960 na tangu hapo sikuwahi kubadili kazi lakini sasa nastaafu ilhali nikiwa
sina hata baiskeli” alisema Gurumo.
Wakati huohuo Mratibu mkongwe nchini wa matamasha mbalimbali
na muanzilishi wav iota na kumbi nyingi
za burudani hapa jijini Dra es Salaam Juma Mbizo anatajwa na Gurumo kuwa ndiye
atakuwa mratibu katika tamasha maalum litakaloandaliwa la kumuaga .
Katika kamati hiyo pia wamo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The African Stars Entertainment ‘Aset’
Asha Baraka, Mdau wa burudani Said Mdoe, Richardson Sakalla, Mkurugenzi wa
bendi ya The Kilimanjaro ‘Wana Njenje’ Waziri Ally.
“Hii kamati imeundwa ili
ili iweze kumsaidia katika kumuandalia tamasha maalum , hivyo ipo
siku tutaweka wazi tumeandaa kumfanyia
nini mkongwe huyu wa dansi kadhalika siku hiyo ya tamasha lake
ndipo atakapoimba kwa mara ya mwisho na kuanzia leo hatopanda katika jukwaa lolote kuimba”
alisema
Mbizo aliongeza kwa kusema kuwa Gurumo amepata ridhaa kutoka
kwa wanamuziki wenzake wote kabla
kufikia uamuzi huo wa kustaafu muziki na kwakuwa ameimba kwa miaka mingi sasa mi wakati wake wa kupumzika.
Wosia wake kwa wanamuziki wanao baki anasema yeye anawaasa
wapige muziki wa nyumbani hasa waliokuwa
wakipiga bendi ya Msondo “Wapige muziki ambao tulikuwa tunapiga sisi
zamani tofauti na hivi sasa ambapo
wanamuziki na vijana wengi wanakimbilia katika muzikiwa Bongo Fleva ambao ni
muziki unaokwenda na wakati lakini ni wa
kupita.
Mwisho anamalizia kwa
kusema kwamba kustaafu kwake hakuzuii
yeye kutoa ushauri au kufundisha wanamuziki na wapiga ala kwani anakipaji cha
kumfundisha mpigaji wa chombo chochote kwa kutumia mdomo wake.
Kadhalika Gurumo anasema kwamba katika nyimbo alizowahi
kuimba wimbo anaoupenda ni wimbo wa ‘Usimchezee
Chatu’ ambao aliumba kipande kidogo mbele ya Waandishi wa Habari na katika wanamuziki wa
Bogo Fleva anampenda Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Gwiji Maalim Gurumo aliyekaa katikati, kushoto ni Meneja wa Bendi ya Msondo Kibiriti na Mratibu wa tamasha Juma Mbizo.Waliosimama ni waandishi wa habari Khadija na Hemed Kivuyo (ITV).Hapa ni mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
0 Comments