WASANII ‘BONGO’ WANASWA NA DAWA ZA KULEVYA BONDENI

MSANII anayeonekana katika  video  nyingi za wasanii za miondoko ya Bongo Fleva hapa Bongo, Agnes Gerald  ‘Masogange’  pichani juu ni kati ya  wanawake walitajwa  kunaswa na  dawa za kulevya  nchini Afrika ya Kusini ‘Bondeni’.
Msanii mwingine  aliyekamatwa  ametambulika  kwa jina la Melisa Edward.Inadaiwa kuwa wasanii hao wameingiza shehena ya  dawa za kulevya zenye thamani ya  zaidi ya sh.bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Taarifa za kuaminika zilitolewa jana kwa waandishi wa habari na Kamanda wa Kitengo Cha kuzuiz dawa za kulevya  nchini Geofrey Nzowa ambaye pia alithibitisha kukamatwa kwa Watanzania hao.
Alisema Melisa na Masogange walikamatwa Juni 5 mwaka huu  nchini humo nab ado wanashikiliwa  na Jeshi la Polisi  na nchi hiyo  kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
“Hadi sasa taarifa  rasmi bado hazijafika hivyo hatujajua  nia aadhabu ya aina gani wanayotumikia tunasubiri taarifa rasmi kutoka Afrika Kusini” alisema Nzowa.
Alisema Jeshi la Polisi nchini kwa upande wake  linaendelea  kufanya uchunguzi  kubaini  kama dawa hizo  walitoka nazo  wapi  na pia linawasaka watu  ambao  watakuwa wamiliki wa dawa hizo.
Habari zilienea katika mitandao ya kijamii  Jumapili iliyopita kwamba wamemamatwa wanawake wa Kitanzania wakiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya bilioni sita  nchiniAfrika Kusini dawa hizi ni aina ya Crystal  methamphetamine.
Taarifa hizo  zilionesha  kuwa wanawake wawili  waliokamatwa  katika Uwanja wa Ndege  wa Kimataifa  wa Oliver Tambo, uliopo eneo la Kempton Park  Ijumaa iliyopita wakitokea Tanzania.
Wanawake hao walikamatwa na Maofisa wa Mamlaka ya Mapato  ya Afrika Kusini , wakiwa na  masanduku  sita ambayo pindi yalipokaguliwa  yalikutwa na kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya  bei ya mtaani  ya Randi milioni 42 sawa n ash. Bilioni 6.8

Post a Comment

0 Comments