NASSIBU RAMADHANI AMTAMBIA JUMA FUNDI



IMG_4971
Promota wa mpambano wa masumbwi Side Mkigoma (katikati) akiwainua mikono juu mabondia Juma Fundi (kushoto) na Nassibu Ramadhani.
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Nassibu Ramadhani amejigamba kuwa atamchakaza mpinzani wake Juma Fundi wakati wa mpambano wao utakaopigwa siku ya Idi pili katika ukumbi wa friends corner Manzese

Aliongeza kwa kusema unajua mimi anaeniumiza kichwa kwa sasa ni Fransic Miyeyusho pekee kwa Tanzania hii kwa kuwa nilicheza nae na nikashindwa kummudu ata hivyo ipo siku nitaomba mpambano mwingine wa marudiano nae hivyo nimemuweka kiporo

Bondia huyo aliendelea kujinasibu kwa kusema kwa sasa mimi ni nambari One hivyo fundi ategemee kipigo cha mbwa mwizi kwa ni ato furukuta
Naomba mashabiki wangu wa ngumi mjitokeze kuja kunishangilia ata kama wewe sio shabiki wango njoo uone ngumi nitakazokuwa nikicheza na utamini kuwa mimi ni kiboko yao

Ramadhani ambaye ucheza kwa kasi kubwa sana awapo ulingoni amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki na kumpachika jina la Mann Paquaio wa Philipins kwa kuwa wote wanatanguliza mguu wa kulia mbele 

Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zatakazokuwa zikisabazwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'

pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi wakisindikiza mpambano huo

Post a Comment

0 Comments