KUNDI LA NGOMA LA EGUMBA WAIBUKA MABINGWA WA BALIMI NGOMA MKOA WA MARA



 Mabingwa wa mashindano ya Balimi  Ngoma Ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Mara,Kikundi cha Egumba wakicheza wakati wa fainali za Ngoma za Asili zilizofanyika katika Bwalo la Magereza   Musoma  mwishoni mwa wiki.Mashindano hayo yanadhaminiwa na TBL kupitia  Bia ya Balimi Extra Lager kwa mikoa ya kanda ya ziwa tu.
Na Mwandishi Wetu.Mara.

KUNDI LA NGOMA LA EGUMBA MABINGWA BALINGOMA MKOA WA MARA.
KUNGI la Ngoma la Egumba wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Ngoma za Asili ngazi ya Mkoa kwa kanda ya Ziwa Mkoa wa Mara yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia Bia ya Balimi Extra Lager Kanda ya Ziwa.
 
Kundi la Ngoma la Egumba kwa ubingwa huo lilijinyakulia kitita cha fedha taslimu shilingi 600,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Mara kwenye fainali za mashindano ya Kanda yatakayojumuisha Mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Tabora,Shinyanga,Kagera,Mwanza na Mara,mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii jijini Mwanza.
 
Katika kinyang'anyilo hicho ambacho kilikuwa na ushindani mkubwa,kundi hilo limeibuka mshindi kwa alama 66.5 likifuatiwa na kundi la Gari kubwa ambalo imepata alama 64 na kuondoka na zawadi ya shilingi laki 5 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Kiwajaki na kujipatia shilingi laki 300 kwa kupata alama 62,
Katika mpambano huo ambao umevishirikisha vikundi 9 na kuhuduriwa na idadi kubwa wa mashabiki wa burudani za ngoma za asili wakiongozwa na Mkuu wa Gereza  Musoma  Edson Yalimo , washiriki wote kuanzia nafasi ya 5 mpaka ya 10 wamejinyakulia zawadi ya fedha tasilimu shilingi laki moja na nusu ambapo mkuu huyo wa Gereza ameipongeza kampuni hiyo kwa kudhamini mashindano hayo ya aina yake hapa nchini.
Mkuu Huyo wa Gereza la Musoma Rpo Edson Yalimo, amesema kuwa kwa kutumia mashindano kama hayo jamii imekuwa ikiburudika na  kutukumbusha tamaduni zetu ambazo mara nyingi zimekuwa zikisahaulika kwa wengi na kuiomba kampuni ya TBL kuendelea kudhamini mashindano hayo na kuwataka kutosita kushilikiana na serikali katika masuala mbalimbali ya kijamii kwa kuwa kwa kufanya hivyo wamekuwa wakisaidia baadhi ya majukumu ya serikali.
Naye Meneja masoko wa  Kampuni ya bia Tanzani (TBL) kanda ya ziwa Endrew Mbwambo amesema kuwa kampuni yake imekuwa ikishiriki katika kudhamini  shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo na burudani ikiwa ni shukrani zao kwa jamii kwa kutumia bidhaa zao ambapo ameiomba jamii ili kampuni hiyo iweze kuendelea kudhamini shughuli hizo wawaunge mkono kwa kutumia bidhaa zao.
Vikundi vingine ambavyo vimeshiriki katika fainali hizo ni pamoja na Nyakitali, Victoria ,Maisha Bora,Musoma One,Mshikamano naKiwasabu ambapo Tarehe 20 mwezi huu itafanyika  fainali hizo katika mkoa wa Mwanza,

Post a Comment

0 Comments