Kushoto meneja wa matukio wa
kampuni ya Bia Tanzania - tbl kanda ya ziwa Bwana Erick Mwayela
akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Tabora Mstahiki Meya Gulamhussein Remtullah
kitita cha shilingi laki sita ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza wa
mashindano ya Ngoma za asili kwa mkoa wa Tabora mashindano hayo yamedhaminiwa
na kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Balimi Extra kulia aliyevaa
fulani ya balimi ni kiongozi wa kundi la Mwenge la manispaa hiyo ambao ndio
wameibuka washindi wa shindano hilo.
Mgeni
rasmi katika mashindano ya ngoma za asili kwa Mkoa wa Tabora Mstahiki
Meya wa manispaa ya Tabora Gulamhussein Remtullah akizungumza na wakazi
wa Mkoa huo katika mashindano hayo chini ya udhamini wa kampuni ya Bia
Tanzania kupitia bia yake ya Balimi Extra , mashindano hayo yamefanyika
katika shule ya sekondari Iyungi
0 Comments