Meneja Mawasiliano wa Barclays, Tunu Kavishe, (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Benki, Kitengo cha Wateja Binafsi, Musa Kitoi wakiwa na washindi wa droo ya pili ya Golden Briefcase Campaign jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Barclyas, Tunu Kavishe (kulia) akiwa na washindi wa pili wa droo ya Golden Briefcase Campaign, Anorld Shirima na Khadija Kashoro.
DAR ES SALAAM, Tanzania
Barclays Tanzania leo imefanya droo yake ya pili ya kampeni ya Maisha Bomba na Barclays Golden Briefcase
kwa wateja wake. Droo hii inawapa fursa wateja 13 kujishindia masanduku 13 ya
dhahabu kwa muda wa miezi mitatu.
Akiongea na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi wa benki, kitengo cha
wateja binafsi, Bwana Musa kitoi alisema, “ Fursa ya ushindi
iko wazi kwa kila mteja (Wateja waliopo na watarajiwa) mwenye akaunti na
Barclays Bank Tanzania. Leo
tumekamilisha droo yetu ya pili na tumewapata washindi 13. Vile vile tunatoa
zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza iliyofanyika tarehe 22 Mei 2013, katika
masanduku kumi na tatu ya dhahabu. Kila mteja atachagua sanduku na kulifungua
ili kuweza kujua zawadi yake. Zawadi zilizopo ni i-Pad, Home theatre, Mashine
za kufulia na vocha za zawadi.
Bwana Kitoi aliongeza na kusema kuwa
“ukiweka pesa zako benki na ukawa na salio lililokusudiwa kwa kipindi cha mwezi
mmoja, wewe ukiwa kama mteja wetu wa sasa na hata yule mpya utaweza kuingia
kwenye droo hii na utapata nafasi ya kujinyakulia zawadi mbalimbali na mshindi
wa jumla atajinyakulia zawadi ya tshs millioni kumi (10,000,000 TZS)” mwisho wa
kampeni. Kampeni hii ilizinduliwa rasmi tarehe11 Aprili 2013 na itaendelea hadi
tarehe 30th June 2013.
Shindano hili liko wazi kwa
wateja binafsi, wapya na wa
zamani, ambao wanaweka fedha zao na
benki yetu hapa Tanzania.
Wateja ambao watatakiwa kuingia katika promosheni hii ni wale tu wenye account
ya hundi (Current Account) au amana
(Savings), na wanatakiwa waongeze salio lao kwenye account kwa shillingi laki
tano za kitanzania (500,000 tzs)au zaidi, na salio hili libakie kwenye account
hadi mwisho wa mwezi bila kupungua, Kila ongezeko la shillingi Laki tano
linampatia mteja ingizo la ziada katika katika droo ya mwezi husika.
Zawadi kubwa ya shilling million kumi za Kitanzania (shs. 10,000,000)
itatolewa mwisho wa kampeni. Zawadi zote zitawekwa kwenye Barclays Golden
Briefcase ambapo kila mshindi atatakiwa kuchagua mojawapo kisha kuifungua ili
kujua alichojishindia. Zawadi
zinazoshindaniwa kila mwezi ni iPads 2, vocha
8 za maduka makubwa ya bidhaa zenye thamani ya shillingi laki 2 kila mmoja
(TZS200, 000), mashine za kuoshea nguo 2, na home theatre 1.
0 Comments