---
MHASIBU
Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts (T) Limited inayochapisha gazeti la
Jambo Leo, Staa Spoti, Dar Metro na jarida la Jambo Brand Tanzania,
Vicky Mgoyo (49), amefariki dunia.
Meneja
Mkuu wa Jambo Concepts, Ramadhani Kibanike, alisema marehemu Vicky
Mgoyo alifariki dunia leo asubuhi kwenye Hospitali ya Kairuki jijini Dar
es Salaam alikokimbimbizwa kupatiwa matibabu baada ya kuzidiwa usiku wa
kuamkia jana
Alisema
kifo cha Vicky zaidi akijulikana kwa jina la Mama Mgoyo kimeacha pengo
kubwa si tu kwa familia yake bali pia kwa Kampuni ya Jambo Concepts
kutokana na kwamba alikuwa ni mtu mwaminifu kazini, lakini pia uhusiano
mzuri na wafanyakazi wenzake.
"Tumepoteza
mfanyakazi ambaye ni mchapa kazi na kipenzi cha wengi, tutamkumbuka kwa
hilo. Naomba wafanyakazi tuungane na ndugu na jamaa katika kuomboleza
msiba wa kipenzi chetu huku tukiamini kuwa haya ni mapenzi ya Mungu.
"Bado
hatujapata taarifa rasmi za maziko, ila taratibu za kusafirisha mwili
wa marehemu kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao zinaendelea
kufanyika," alibainisha Kibanike.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Juma Pito alitoa mwito kwa wafanyakazi
kuonesha mshikamano katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi kwa
kuondokewa na mfanyakazi mwenzao.
Mhariri
Mkuu wa Jambo Leo, Anicetus Mwesa, akizungumzia msiba huo alisema Mama
Mgoyo ametwaliwa na Mungu ilhali akiwa bado anahitajika na familia
pamoja na ofisi yake, hivyo ameacha pengo ambalo litachukua muda
kuliziba.
"Mwenzetu ametangulia nasi tupo nyuma yake, zaidi tumwombee ili Mungu ampumzishe katika raha ya milele," alisema Mwesa.
Kwa
upande wake Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hili, Richard Mwaikenda, alisema
atamkumbuka Vicky kwa kuwa ni mwanamke shupavu ambaye alikuwa
anazingatia maadili ya kazi yake ya uhasibu.
Pia
alisema alikuwa ni mama mjane makini ambaye alihakikisha anasimamia
watoto wake katika suala la kuwapa elimu bora, ambapo katika hilo
alikuwa akifanya kila anachoweza kuhakikisha anasomesha nje ya nchi tena
kwenye shule bora na makini.
Vicky Mgoyo aliyezaliwa Novemba 26, 1964, ameacha watoto watatu huku wawili kati yao ni wanaume.
Alilazwa
katika Hospitali ya Kairuki wiki iliyopita ambako alipatiwa matibabu
kwa muda wa siku nne na kuruhusiwa.Jumatatu aliripoti kazini na
kuendelea na kazi hadi jana jioni, ambapo usiku alizidiwa na hatimaye jana asubuhi Mungu alimchukua. Mungu ailaze pema peponi roho ya Vicky Mgoyo.
0 Comments