Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited
(TDL), David Mgwassa (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari, Dar es Salaam jana, ambapo alilalamikia kitendo cha baadhi ya
magazeti yenye uhusiano wa nchi jirani, yanayotumika kuchafua bidhaa za
TDL. Kushoto ni Meneja Masoko wa TDL, Joseph Chibehe.
Tumeanza kuona magazeti yenye affiliation na nchi za jirani yakitumika ku misrepresent products za TDL.
Articles ninazozungumzia zilichapishwa tarehe 2 may 2013 na tarehe 6 may
2013, kupotosha umma, na kupindisha ukweli. kwa sababu mawasiliano ya
kisheria yanafanyika sitataja ni magazeti gani yanahusika, lakini nina
uhakika yana uhusiano mkubwa wa kibiashara na nchi jirani.
Ushauri wangu ni kuwa magazeti ya Tanzania, yaepukane sana na vitu
vinavyoonyesha kuwa kuna muelekeo wa kurepresent matakwa ya nchi tofauti
na kupuuza matakwa ya kitanzania
Kitendo cha kujaribu kuoanisha brand ya Konyagi na accidents za magari au piki piki , ni ya
upotoshaji mkubwa wa jamii ya kitanzania, kwani hakuna bia, hakuna pombe za kienyeji au pombe kali. Huu ni uhuni na ujinga mtupu
Sisi TDL hatuogopi ushindani, sio ushindani wa humu Tanzania, na nasema
tutaendelea kuuza products zetu zinazozalishwa Tanzania, huko Uganda,
Kenya south Sudan, Rwanda na Burundi, licha ya matatizo makubwa
tunayopata
Na tutaendelea kuwasiliana na mabalozi, wa nchi husika, EAC office na
wizara zenye mamlaka katika kukuza soko la pamoja la Jumuia ya Afrika ya
Mashariki, kuhusu changamoto za kibiashara tunazozipata.
Kama nilivyozungumza mwanzo sisi hatuzalishi Konyagi tuu, bali
tunazalisha Zanzi cream, Knights, Viceroy brandy , siyo kwa sababu
hatuwezi kuagiza, bali wka kutumia watanzania katika uzalishaji na
kuwapa ajira. Msitufananishe sisi na watu wanaoleta makatoni ya pombe
kutoka Ireland au uingereza, sisi tuko tofauti na mahitaji ya nchi hii
tunayajua.
Raisi wetu Dr Kikwete kila siku anasema issue hiyo hiyo, value added , value added, mbona masikio yenu mnafunga?
Naomba niwaeleze ukienda South Africa leo utaona kila aina ya magari
mapya, utaona Toyota, utaona Nissan utaona Mercedez benz , utaona Kia na
kadhalika, lakini magari yote hayo yanaundwa South Afrika, huwezi
kukuta gari imetengenezewa Singapore, nia ni kuhakikisha kuwa wenyeji
wanapata kazi, na approach yetu TDL ni same.
Sioni kati ya nyie mtu ambaye anamchukua mtoto wake kumpeleka Nairobi au
Dubai, kumtafutia kazi, wote mnawaleta kwetu, hata leo wengine
wananiomba kazi, kwa hiyo naomba sana mtu akikujaza akili au upumbavu,
na wewe jaribu kuchanganya na akili nzuri za kwako
Ahsanteni sana |
|
|
0 Comments