ASHANTI UNITED YAFANYA KUFURU




Mgeni rasmi Edson Fungo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la Napoli


Wageni wakitazama wanachama wakicheza pamoja na matarumbeta (hawapo kwenye picha)


Baadhi ya wachezaji wa Ashanti wakiwa wapo pamoja na wanachama wa Ashanti


Ashanti haichagui rangi kwani haina wenyewe, wenyewe ni wale wote wenye mapenzi mema nayo

Almas Kasongo ambaye ni  Mwenyekiti wa DRFA akiongea kwenye hafla hiyo

Khalfan Suleiman akitoa maoni yake

Rais wa tawi la Napoli Ally Mahmoud akiwa amebebwa na wanachama wa tawi hilo 

Wanachama wa Napoli

Ally Mahmoud, Rais wa tawi la Napoli akiongea
Mwanachama akipokea kadi yake

Mwenye kiti wa serikali za mitaa akipokea kadi yake

Wachezaji na baadhi ya mashabiki wakiwa na kocha Mubaraka Hassan

Wachezaji na benchi la Ufundi

Mgeni rasmi akiwapongeza wachezaji kwa kuwashika mikono

Almas Kasongo

Mgeni rasmi Diwani wa Ilala, Edson Fungo akiongea na wanachama na mashabiki wa Ashanti


Mgeni rasmi akipata maakuli pamoja na wenyeji wake 

Biriani tamu hadi wanalisikilizia


Wachezaji nao hawakuwa nyuma, cheki plate zilivyojaa halafu mmoja kakamatia peke yake








WANACHAMA wa timu ya Ashanti  United inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, msimu ujao wamezindua tawi la kwanza kuanzia timu hiyo ianzishwe kwa ajili ya kutoa hamasa na kuiwezesha kiuchumi timu hiyo jana.
Tawi hilo linaitwa Napoli na lina wanachama 55 limezinduliwa kwenye mtaa wa Kilwa na Utete, Ilala na Diwani wa Kata ya Ilala kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Edson Fungo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyohudhuriwa na wachezaji wa Ashanti, wanachama na viongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Edson Fungo ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, aliwataka wanachama hao kufuata katiba ya timu na siyo kuendesha tawi kwa manufaa yao bali ya klabu.
“Nimefurahi kuona mmeguswa na kuanzisha tawi hili hivyo na mimi nitakuwa mwanachama, lakini msiache majukumu yenu kama wanachama badala ya kusaidia Ashanti mkajisaidia wenyewe na kuleta migogoro”, alisema Fungo.
Pia aliwataka wachezaji wacheze kwa kujituma wakijua kuwa mpira ndio ajira yao ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Almas Kasongo alisema amefurahishwa na wanachama hao kuona wanawiwa  kuona Ashanti inafanya vizuri na kuwaahidi atakuwa pamoja nao ili Ashanti isiwe inakwenda kucheza ligi kuu  na baadae kurudi tena daraja la kwanza.
Naye Rais wa tawi hilo la Napoli, Ally Mahmoud alisema kuwa tawi lao litakuwa na kazi ya kuisaidia timu kiuchumi kwani wanachama watakuwa wanalipa ada ambazo zitakuwa zinakwenda kusaidia timu.
“Mpira unaendesha kwa kutumia pesa hivyo sisi kama mashabiki wa Ashanti tumeguswa tukaona namna ya kuisaidia timu ni kuanzisha tawi hili ili kila mwanachama achangie timu”, alisema Mahmoud.
Wanachama wa tawi hilo walikabidhiwa kadi zao kisasa  na mgeni rasmi na kuahidi kuwa wanachama watiifu kwa uongozi na timu yao.

Post a Comment

0 Comments