UKUMBI WA MASUMBWI KUHAMIA CHALINZE


Bondia Martin Shekivuli kushoto akipambana na Abdull Ndosa wakati wa mpambano wao wa kirafiki ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mpambano huo ulitoka droo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Amour Mzungu katikati akipambana na Josefu Marwa wakati wa mpambano wao wa kirafiki uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kushoto ni refarii Ibrahimu Kamwe Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Refarii Ibrahimu Kamwe akimnyoosha mkono juu Amour Mzungu kuwa mshindi wa mpambano huo dhidi ya Josefu Marwa Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar katikati akizungumza mbele ya mabondia Issa Omari kushoto na Shabani Madilu kabla ya mpambano wao Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
  
Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar
Diwani wa Kata ya Bwilingu Chalinze Bagamoyo,Ahmed Karama Nassar amesema yupo tayali kushilikiana na wadau mbalimbali ili iwezekane kupatikana ukumbi maalumu wa mchezo wa masumbwi Chalinze aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika mapambano ya ngumi yaliyopigwa katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala

Nina tarajia kufikisha mbali mchezo huu kwa kuwa mmenishawishi kuupenda mchezo wa masumbwi mchezo unaopendwa na wengi na kukimbiwa na wadhamini wachache ata hivyo nimeandaa mpambano rasmi utakaochezwa Chalinze kwa ajili ya kuhamasisha mchezo huu siku ya April 21 hivyo nawaomba wadau wote wa ngumi tuamie chalinze kwa mda hili tuweze kuhamasha mchezo huu

Ambapo siku hiyo kutakuwa na ushindani mkubwa wa mabondia kutoka Dar es salaam watacheza na mabondia wa Chalinze siku hiyo ata hivyo kwa kuonesha kwamba anajili na anathamini mchezo wa masumbwi ame aidi kutoa gari moja kwa ajili ya mashabiki na mabondia kwenda kushiriki mchezo uho wa April 21

mbali na ahadi hiyo Diwani huyo ametoa pesa taslimu shilingi 1,50000 kwa ajili ya malipo ya baadhi ya mabondia waliokuwa awajilipwa na kuanza kudai kabla ya kupanda ulingoni na kuhamua kuchukua jukumu hilo la kuwalipa mabondia hao

Mmoja ya wadau wa mchezo wa masumbwi nchini Ibrahimu Kamwe  amesema kuwa yupo tayali kutoa ushilikiano wa hali na mali kwa kuanzia atachukua baahi ya vijana kwa ajili ya kwenda kucheza mchezo wa masumbwi uliopangwa siku hiyo hivyo tupo pamoja unajua ngumi watu wanapenda kuangalia ili galama zake ni kubwa ata hivyo naona ajabu wadhamini kushindwa kujitokeza kuzamini mchezo huu unaopendwa na vijana wengi

na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa Ahmed Karama Nassar kwa kuanza kusapoti mchezo wa masumbwi sehemu uliyopo

Post a Comment

0 Comments