Profesa
Lipumba, akiangalia ukuta uliojengwa na wananchi wa Kijiji cha Kigombe
mkoani Tanga, mara baada ya kuuzindiwa, kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji
hicho Mzee Said.
Mwandishi Wetu, Tanga
MWENYEKITI
wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Mkoa wa
Tanga ni moja kati ya mikoa maarufu kwa viwanda nchini lakini hivi saa
hali ya kimaendeleo katika mkoa huo imekuwa mbaya.
Kauli
hiyo ameitoa leo mjini hapa alipokuwa akiwasilisha mada inayohusu
maendeleo ya uchumi kwa Mkoa wa Tanga katika kongamano lililoandaliwa na
Chama cha Wananchi (CUF) kwa kushirikiana Taasisi ya Maendeleo ya
demokrasi kwa vyama vya siasa ya nchini Denmark (DIPD).
Profesa Lipumba alisema kuwa hakuna haki bila kuwa na maendeleo yanamgusa mwananchi wa kawaida.
Alisema
Mkoa wa Tanga imefanikiwa kuwa na rasimali nyingi ikiwemo zao la Mkonge
ambalo kwa sasa limekosa msukomo hali inayochangia umaskini kwa
wananchi wa mkoa huo.
"Pamoja
na Tanga kuwa na fursa nyingi za kiuchumi lakini bado kadri siku
zinavyokwenda umaskini umekuwa ukiwatesa wananchi. Viwanda vilikuwa
zaidi ya 70 lakini sasa hakuna hata kimoja kinachofanya kazi huku zao la
mkonge lilikosa msukumo wa makusudi kwa wananchi wake.
"Katika
soko la dunia inaonyesha kuwa Tanga ilikuwa ikizalisha tani 234,000 kwa
mwaka lakini sasa mkonge umeporomoka na kufikia tani 25,000 tu hali
ambayo imekuwa ikiongeza umaskini kila kukicha. Kama kungekuwa na
msukumo wa makusudi wa kufufu zao hili ni wazi Tanga ingekuwa imepaa
kimaendelo kwa wananchi wake kutokana na kuwa na kila aina ya rasilimali
zikiwemo za matunda na mbogamboga," alisema Profesa Lipumba.
Profesa
Lipumba, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi duniani, alisema ili
kuweza kufikia malengo ya mkoa huo kuweza kupambana na umaskini ni
lazima serikali ikubali kwa kufanya uwekezaji hasa katika kufungua
bandari ya Tanga ambayo ni lango kuu la kiuchumi.
Alisema
Bandari ya Tanga imekuwa haitumiki ipasavyo hali inawechangia kwa kiasi
kikubwa kuongezeka kwa umaskini na hazorotesha harakati za mkoa na
wananchi kwa ujumla.
"Bandari
ya Tanga, zao la mkonge pamoja na kukosekana kwa msukumo wa kuimarisha
sekta ya elimu ni moja ya masuala yanayoufanya mkoa huu kuzidi kurudi
nyuma kiuchumi pamoja na wananchi wake,” alisema Profesa Lipumba
0 Comments