TFF YAWAPONGEZA WAANDISHI WALIOSHINDA TUZO YA EJAT



Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akimkabidhi Tuzo ya Mwandishi Bora wa Michezo kwa upande wa Radio, Abdalah Majura, wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT),  (Picha na Habari Mseto Blog)
DAR ES SALAAM, Tanzania

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewapongeza waandishi watatu wa habari za michezo k
wa kushinda Tuzo ya Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) inayotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
Waandishi hao walioshinda katika kategori ya michezo na utamaduni ni Abdul Mohammed wa The African kwa upande wa magazeti na Abdallah Majura wa redio ABM kwa upande wa redio.
TFF tunawapongeza kwa ushindi huo uliotokana na makala zao ambazo zina mchango katika maendeleo ya mpira wa miguu, lakini pia ni changamoto kwa waandishi wengine ambao hawakufanikiwa kushinda.
Vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika ustawi wa michezo ukiwemo mpira wa miguu, kwani katika nchi nyingine vimefichua rushwa. Ni matarajio yetu kuwa vyombo vya habari nchini navyo vitakuwa mstari wa mbele katika kufichua na kupambana na rushwa katika mpira wa miguu.
MECHI YA AZAM, BARRACK YAINGIZA MIL 44/-
MECHI ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam ya Tanzania na Barrack Young Controllers II ya Liberia iliyochezwa jana (Aprili 6 mwaka huu) imeingiza sh. 44,229,000.
Fedha hizo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 17,128 waliokata tiketi.
Viingilio vilikuwa sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A. Kiingilio cha sh. 2,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 15,212.
Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya uwanja sh. 5,798,025, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 3,865,350 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh. 28,990,500.
Mechi iliyopita ya raundi ya awali ya mashindano hayo kati ya Azam na El Nasir ya Sudan Kusini iliyochezwa kwenye uwanja huo huo Februari 16 mwaka huu iliingiza sh. 34,046,000 kwa viingilio hivyo hivyo huku ikishuhudiwa na watazamaji 13,431.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Post a Comment

0 Comments