Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Kilimanjaro, Iddi Mohammed baada ya kuwasilili jioni hii kwenye
Ofisi ya CCM mkoa huo mjini Moshi. Kesho Nape anatarajiwa kufungua
semina ya Halmashauri Kuu ya Mkoa huo ya CCM na baadaye kuhutubia
mkutano mkubwa wa hadhara mjini Moshi.
Katibu
wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Steven Kazidi (wapili kushoto)
akimtambulisha Mwenyekiti wa UVCCM mkoa huo, Frederick Mushi kwa Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa
Kilimanjaro mjini Moshi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini
Elizabeth Minde.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akivishwa skafu na Kijana wa CCM
baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanajro mjini Moshi jioni
hii.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kucharaza ngoma,
iliyokuwa inapigwa na kundi la sanaa la CCM, baada ya kuwasili kwenye
Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro jini Moshi jioni hii.
Katika
ziara hiyo Nape ameambatana na Vijana waliojiengua hivi karibu kutoka
Chadema, Mtela Mwampanga na aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la
Vijana Chadema, Juliana Shonza. Pichani, Mwampamba na Shonza
wakisalimiana na vijana wenzao ambao pia wamehamia CCM hivi karibuni
kutoka Chadema mkoani Kilimanjaro, David Waryoba (kushoto) na Yona
Makwaya (wapili kushoto)
Vijana wakimsubiri Nape kwa shauku alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi jioni hii.
Nape
akitia saini kwenye kitabu cha wageni, katika Ofisi ya CCM mkoa wa
Kilimanjaro mjini Moshi jioni hii. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Kilimanjaro Iddi Mohammed. (Picha zote na Bashir Nkoromo wa NKOROMO BLOG
0 Comments