BLOGGERS FC YAISAMBARATISHA DSJ KWA MAGOLI 3 KWA 2 KATIKA MICHUANO YA MEDIA DAY INAYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS



Hiki ndio kikosi cha Bloggers FC kilichoisambaratisha DSJ kwa magoli 3 kwa 2 Dhidi ya Timu ya DSJ katika Michuano ya Media day inayoendelea kufanyika katika viwanja vya leaders clubs jioni hii kulia ni kocha wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D'  ambaye ni mmiliki wa blog ya www.superdboxingcoach.blogspot.com
Wachezaji wa Bloggers Fc (wenye jezi za blue) wakichuana na wachezaji wa DSJ langoni mwa timu ya DSJ wakati timu hizo zikichuana katika michuano ya MEDIA day inayofanyika katika viwanja vya leaders jioni hii
Mchezaji wa Bloggers FC Josephat Lukaza (aliyeshika nguzo ya goli) akimsadia mlinda mlango wake Othman Michuzi (mwenye jezi ya njano) katika kuokoa hatari iliyopigwa langoni mwa timu ya bloggers fc na wachezaji wa DSJ katika michuano ya media day inayofanyika katika viwanja vya leaders jioni hii

Hiki ndio kikosi cha Bloggers FC
Mchezaji wa DSJ akijaribu kupeleka mashambulizi langoni mwa Bloggers fc bila mafanikio katika michuano ya Media day inayofanyika jioni hii katika viwanja vya leaders club

Post a Comment

0 Comments