Washiriki wa Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13, jana wametembelea
Ukumbi wa kwanza na wa Kisasa na wa aina yake Tanzania ambao
unamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kurugenzi ya mambo
ya kale na makumbusho ya Taifa uliopo ndani ya Makumbusho ya Taifa
jirani na Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) karibu na maeneo ya Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Wakiwa
katika Ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua watu 470 kwa wakati mmoja,
walishuhudia Viti, Mitambo na vifaa vingine vya kisasa vyenye uwezo wa
kuendesha Matamasha na mashindano ya Urembo kwa kiwango cha hadhi ya
nyota tano.
Wengi
wa washiriki hao walionyesha hamasa na kujaribu kuwashawishi viongozi
na wakuu wa msafara wao ili kufanya Fainali hizo katika Ukumbi huo ambao
umekuwa ni kivutio kikubwa, jambo ambalo Viongozi na kamati iliokuwa na
jopo la msafara huo lilionekana kukubaliana na mawazo ya nia ya warembo
hao ya kuomba Fainali hizo zifanyike ndani ya Ukumbi huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano hayo
nchini na Barani Afrika Erasto G. Chipungahelo,kuhusu uwezekano wa
kuandaa Fainali hizo katika Ukumbi huo wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM THEATRE, alisema
kuwa kila jambo ni mipango, hivyo na kwa kuwa lengo na nia ya
Mashindano ya Miss Utalii ni kutangaza Vivutio vya Taifa kuna uwezekano
pia Fainali hizo zikafanyika hapo ikiwa pia ni kuwapa heshima Wizara ya
Maliasili na Utalii ambao ndiyo walezi wakuu wa mashindano ya Miss
Utalii Tanzania kwa kuwa wao ndiyo wamiliki wa Ukumbi huo ambao kwa sasa
unaonekana kuwa ni kati ya kumbi pekee zilizojengwa kisasa na hadhi ya
kimataifa hapa nchini Tanzania.
ziara hiyo ya kutembelea Ukumbi huo kwa washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/2013 iliandaliwa na Washiriki wenyewe baada ya kuusikia sifa zake kutoka kwa watu mbalimbali na Mitandao ya Kijamii.
Aidha
Chipungahelo amesema kwamba warembo hao wanatarajia kupanda katika
jukwaani baada ya kutoka kwenye ziara ya kutembelea hifadhi za Taifa
ambazo ni pamoja na Saadan, Mikumi, Udzungwa, Mkomanzi, Arusha na Mlima
Kilimanjaro watakaokuwa wameambatana na waandishi wa habari.
Akizungumzia hali ya Ukumbi huo
Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo amesema kwamba ni
heshima kubwa kwa Taifa na sekta nzima ya Utalii kuona Warembo ambao
wanatangaza Utalii wa Nchi yetu wakivutiwa na
ukumbi huo hata kufikia kupeleka maombi ya kutaka wao kuwa Warembo wa
kwanza kupanda katika jukwaa hilo la Ukumbi wa kisasa na wa kimataifa wa
NATIONAL MUSIUM THEATRE ulipo ndani ya Makumbusho ya Taifa ambao ni kivutio kikubwa kwa sasa katika anga za Burudani na sanaa.
“Ukumbi
ni mzuri kama ambavyo wenyewe wandishi mlivyoona na kutazama, hakika ni
jambo la kujivunia na kusifiwa kwa Wizara yetu, maana unaonekana ni
jambo la kujipanga hadi kuweza kutengeneza kwa ubora huo unaoonekana
sasa, bila shaka nyie wenyewe mtaona ni kwa kiasi gani Umeandaliwa,
lakini hata hivyo ni changamoto kwa Wizara zingine katika kubuni na
kuweka rasilimali kama hizi kwa manufaa ya Taifa, kama ambavyo mnaona
wenyewe, kwani hata Washiriki wamefurahi na hata kusifia sana hivyo pia
nachukua fulsa hii kuishukuru Wizara kwa kuwekeza Ukumbi wa Kisasa ambao
ni faida kwa Taifa” alisema Chipungahelo.
Pia
aliendelea kusisitiza na kuomba wadau na wapenzi mbalimbali wa
mashindano haya kujitokeza kuunga mkono kudhamini na kununua tiketi siku
ya shindano..
Erasto G. Chipungahelo
Rais – Miss Tourism tanzania Organisation
0 Comments