Waziri Mkuu alikuwa akutane na Waandishi
leo saa tisa alasiri. Kutokana na kikao kirefu cha madiwani wa Manispaa ya
Mtwara/Mikindani na Mtwara vijijini pamoja na kikao cha wafanyabiashara,
majumuisho ya ziara ya Mtwara atayatolea ufafanuzi kesho. Kwa sasa anakula
chakula na kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mtwara kitafuatia. Kutokana
na kuwepo kwa makundi katika Kamati ya siasa ya CCM mkoa, wabashiri wengi
wanasema kikao hicho kitakuwa na mvutano mkali.
Dondoo
Muhimu
*Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa bomba
la gesi kwenda Dar.
*Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka
Waziri Mkuu aondoke naye.
*Wajumbe (Madiwani ) kumpinga kwa kauli
moja Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa
kutumia mamlaka yake kutoa kauli za uongo
kuhusu Mtwara vijijini kuunga mkono suala la gesi kusafirishwa kwenda Dar, Madiwani wa Mtwara
vijijini wamesema hawakushirikishwa.
*Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani na Mkuu wa Wilaya
*Waziri Mkuu kutumia mbinu ya kisiasa kuwashawishi bomba liende Dar
*Wajumbe wameondoka kwa shingo upande kwa kukubali kutokubaliana na
Waziri Mkuu.
*Kikao kinafanyika chini ya ulinzi Mkali wa FFU, JWTZ na Usalama wa
Taifa.
*Hawa Ghasia arudishwa uwanja wa Ndege JKNIA asije Mtwara kwani anaweza
kuchafua hali ya hewa.
*Polisi wanadai Meya anataka kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana
na kauli yake ya kusema wao ndio
chanzo cha vurugu.
|
0 Comments