Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga,
Ernest Brandts amesema timu yake itafanya vizuri katika mechi ya
marudiano ya kirafiki dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini
niliyopangwa kufanyika jumatano mjini Mwanza.
Brandts alisema wachezaji wake
wote wamefikia kiwango kile anachotaka na mchezo huo utakuwa muhimu
sana kwake kwani ni wa mwisho kabla ya kuingia katika kampeni za kutwaa
ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Alisema kuwa Black Leopards ni
timu nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza
iliyofanyika kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.
“Ni mechi nzuri ambayo nadhani
itakuwa ni kipimo kikubwa kabla ya kuanza kwa LigiKuu ya Tanzania Bara,
wachezaji wangu wana viwango vizuri sana kwa sasa na naamini makosa
yaliyofanyika katika mechi ya kwanza hawatayafanya tena,” alisema
Brandts.
Kuhusiana na mabacha wawili,
Mbuyu Twite na Kabanga Twite kucheza upande wa kulia, Brandts alisema
kuwa wachezaji hao wana uwezo wa kucheza nafasi nyingi katika timu yake
na uamuzi huo ulikuwa na faida kwa Yanga.
“Kabanga anauwezo wa kucheza
nafasi ya ushambuliaji, katikati, beki zote na hata Mbuyu ana uwezo huo,
hivyo uwepo wao katika timu ni mkubwa, niliwapumzisha kutokana na
mipango ya mechi na wala si vinginevyo,” alisema.
Msemaji wa Klabu Yanga, Baraka
Kizuguto alisema jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya maandalizi ya
Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pia wameamua kuicheza ili kuwapa burudani
mashabiki wa Mwanza.
Kizuguto alisema kuwa Yanga
haitakuwa na mechi yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya ziwa na hiyo
ndiyo nafasi yao ya kuwapa waonyesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa
Mwanza nini wamekipata kutoka Uturuki.
“Tuna mashabiki wengi sana
Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu kwani mahsbaiki
na wanachama watapata fursa ya kuona kiwango na maandalizi ya timu yao
kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili,” alisema Kizuguto.
0 Comments