UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TPBC TAREHE 12 JANUARI, 2013

                                                                                   WANACHAMA,

                                                                   TANZANIA PROFESSIONAL BOXING COMMISSION,
                                                                    S. L. POSTA 6058,
                                                                    DAR ES SALAAM.
 
Kumb. Na: CP/MO/3                                                 24 Novemba, 2012
 
Msajili wa Vyama,
Wizara ya Mambo ya Ndani,
S. L. Posta 9223,
DAR ES SALAAM.
 
Ndugu,
 
YAH: TAARIFA YA KUFANYA MKUTANO TAREHE 12 JANUARI, 2013.
 
Rejea barua yako Kumb. Na: S.O. 6446/17 ya 23 Agosti, 2011 iliyotujibu kuhusu mwongozo wa kukufufua chama chetu, kwa kutufahamisha kuwa ombi hilo haliwezi kushughulikiwa kabla haijalipwa ada ya usajili na adhabu ya kutolipa kwa miaka ya fedha 1998 mpaka 2012. Aidha rejea pia barua yako Kumb. Na: S.O. 6446/20 ya
13 Septemba, 2011 iliyosisitiza barua yako Kumb. Na: S.O. 6446/17 ya 23 Agosti, 2011.
 
Malipo yamekwisha kufanywa na wanachama hivyo tumepanga kufanya mkutano tarehe 12 Januari, 2013 wa kuhakiki wanachama na kufanya uchaguzi wa viongozi wa muda:
 
[1] UONGOZI WA CHAMA:
 
       Chama hakijawahi kufanya uchaguzi wowote ule kikiwa hai au kimekufa    
       tangu mwaka 1998 kilipowachagua viongozi :
            [a] Emmanuel Salehe       – Rais wa chama
            [b] Onesmo Ngowi           - Makamu wa rais wa chama
            [c] Fidel Haynes                 - Katibu Mkuu
            [d] Titus Kadyanji              - Mweka Hazina
            [e] Habibu Kinyogoli        - Mjumbe
            [f] Bakari seleman                        -  Mjumbe
 
        Tarehe 12/01/2000 mkutano mkuu wa chama ulimthibitisha Onesmo Ngowi
        kama rais wa chama.    
 
        Viongozi wote aliochaguliwa 1998 wapo hai kasoro Bakari Selemani ambaye
   ni marehemu lakini hawajishughulishi na maswala ya chama. Badala yake
   Onesmo Ngowi amekuwa akitoa madaraka anavyotaka yeye hata kwa watu
   ambao hawana sifa ya kuwa wanachama. Chama hiki ni cha mabondia.
 
[2] OFISI YA CHAMA
      Chama hakina ofisi wala mahali maalum pa kukutania.
 
      Mabondia wapokuwa na shida huambiwa na Onesmo  
      Ngowi kuwa wakamtafute Boniface Wambura ambaye kama mwandishi wa  
      habari hana sifa za kuwa mwanachama.
 
[3] MIKUTANO YA CHAMA:
 
      Mkutano Mkuu wa mwisho wa chama ulifanyika mwaka 2001 ambao
      ulizungumzia mabadiliko ya katiba ambayo ilitaka kuwaondolea mabondia
      uwanachama.
      Kwa pamoja walipinga hili kwa kuwa hiki ni chama kilichosajiliwa na mabondia
      kwa ajilia ya mabondia na wala siyo kampuni ya mtu.
 
[4] MAPATO NA MATUMIZI:
 
Taarifa ya mwisho ya mapato na matumizi ililetewa kwa wanachama tarehe
31 Desemba, 2000. ( AMBATANISHO NA: 1 )
 
Lakini katika miaka yote hii 12 mabondia wamekuwa wakikatwa asilimia kumi
( 10%) ya malipo yao kila waposhindana nje ya nchi aidha mapromota wamekuwa wakilipia vibali vya kuandaa mapambano.
 
[5] WANACHAMA:
 
       Chama tulikianzisha kwa ajili ya mabondia mwaka 1984 na orodha ya
       wanachama mpaka mwaka 1998 ambayo ndiyo iliyofanya uchaguzi wa 
       mwisho ( AMBATANISHO NA:2 )
 
[6] DHANA YA KUITISHA MKUTANO
Wanachama tuliona kuwa sababu ya malimbikizo ya ada ya usajili ni kuwa hakukuwa na mtu wa kuwajibika kuhusu hili. Ndio maana tukalipia.
 
     Aidha kukosekana kwa [a]  ofisi [b] takwimu ya  mapato na matumizi [c]
     orodha ya wanachama na [ d] viongozi wa chama wa kuwajibishwa.
 
Hivyo basi iwapo una pingamizi kuhusu mkutano huu basi tunaomba mwongozo wako.
 
Wako mtiifu,
 
_______________                                              __________________
Chaurembo Palasa                                              Agapeter Mnazareth
MWENYEKITI WA MKUTANO                           MJUMBE
 
Nakala kwa: [1] Vyombo vya Habari 

Post a Comment

0 Comments